Thursday, October 8, 2015

TAMUNET YAFANYA MKUTANO

Wa kwanza kushoto, Abraham Kapinga (Tanzanite Band) Katibu Mkuu wa Mtandao

Toka kushoto-Innocent Nganyagwa, Ally Jamwaka(Sikinde), Rashid Pembe(Mark Band), Davidi Ng'asi(Mwalimu wa muziki)

Abdul Salvador
Wanamuziki kadhaa walikusanyika jana kwenye ofisi za TAMUNET, Tanzania Musicians Network kujadili mambo kadhaa yanayohusu wanachama wa Mtandao huo. Baadhi ya mambo yalitojadiliwa ni tathmini ya wanamuziki kujiunga na Bima ya Afya, Tamasha la sanaa litakalokuweko March 2016 huko Ivory Coast, ushiriki wa Mtandao katika uboreshaji wa elimu ya muziki, na pia kuangalia nafasi ya maendeleo ya muziki katika serikali ijayo.
Ilionekana kuwa kasi ya kujiunga na bima ya afya bado ni ndogo, na moja ya sababu ni ukosefu wa uelewa kuhusu umuhimu wa Bima na namna ya utendaji wa Bima. Mikakati ilipangwa kukabili hali hiyo.
Taaarifa ya Tamasha ilikwisha anza kusambazwa kutumia mitandao ya Facebook, vikundi vya Whatsapp Blog hii na taarifa za mdomo. Tayari wasanii kadhaa walionyesha nia ya kushiriki. Mtandao uangalie namna ya kwezesha wanamuziki hawa kufanikiwa katika ushiriki wa tamasha hili.
Ilikuablika kuwa katika wiki mbili zijazo kufanyike kikao cha kuangalia utekelezaji wa kushiriki katika kuboresha elimu ya muziki. Mwanamuziki na Mwalimu wa Muziki David Ng'asi alipewa jukumu la kuja na andiko la awali la mkakati huo.

No comments:

Post a Comment