Thursday, November 23, 2017

MTANDAO WA MUZIKI WAMPONGEZA MSAMA

Msama

Kitime
Mtandao wa Muziki Tanzania  umempa hongera  Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart
 kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiendelea nayo muda mrefu ya kukamata wezi wa kazi za muziki na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kupunguza uharamia na kuhamasisha uchangiaji wa pato la Taifa kupitia kazi za sanaa. Katika pongezi hizo Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime amesema'Kwa niaba ya wanachama wa chama chetu Tanzania Musicians Network, naomba nitoe shukrani kwa mchango wako mkubwa ambao kampuni yako inaufanya katika jitihada za kupunguza uharamia wa kazi za sanaa Dar es Salaam.  Tuko tayari kushirikiana nawe kila wakati kwa lengo la kuboresha mazingira yanayohusu uboreshwaji wa stahiki za wanamuziki wakati wowote.Tunarudia tena kushukuru kwa hili'
Msama amekuwa akifanya kazi hii ya kukamata kazi zisizo halali kwa miaka mingi, na Kitime amekuwa mwanaharakati wa swala la Hakimiliki kwa miaka mingi pia.

Friday, November 10, 2017

SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA LAJIANDA KUTENGENEZA DATABASE YA WANAMUZIKI TANZANIA


Shirikisho la Muziki Tanzania ambalo ni muungano wa vyama vya muziki, jana 9/11/2017,  lilifanya warsha ya kuchambua makubaliano na kampuni ya COGSNET Technologies Ltd ili kuweka mazingira ya kuingia mkataba na kampuni hiyo kwa shughuli ya kuunda Database ya wanamuziki Tanzania.
Mkakati huo ambao ulibuniwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Mwakyembe mwezi mmoja uliopita,  uliongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Addo November na Katibu Mkuu John Kitime na hatimae kuweza kufikia hatua ya kukutanisha viongozi wa vyama vyote na kukubaliana umuhimu wa kazi hiyo. Uchambuzi ulichukua zaidi ya saa 7 ambapo wawakilishi 32 kutoka vyama vya muziki 6 walishiriki. Vyama hivyo vilikuwa Chama cha Muziki wa Injili (CHAMUITA), Chama cha Muziki wa Dansi (CHAMUDATA), Chama cha muziki wa Kizazi kipya (TUMA), Chama cha muziki wa rumba (CHAMRUTA), Chama cha Muziki wa Disco (TDMA), Chama cha Madansa (TDA).
 Viongozi wa vyama hivi kwa pamoja walichambua makabrasha mbalimbali yatakayowezesha Shirikisho kuingia mkataba wa kuanza kupata idadi na taarifa kamili za wanamuziki na kazi zao nchini Tanzania. Zoezi hili litakapoanza litafanyika nchi nzima na wanamuziki wa aina zote wataingizwa katika Database na hivyo kutoa picha halisi ya shughuli za muziki nchini na pia kusaidia wanamuziki katika namna mbalimbali ikiwemo kuwarahisishia biashara ya kazi zao.




Viongozi wa vyama mbalimbali vya muziki


Viongozi na wanachama wa vyama vya muziki

Monday, October 30, 2017

Waziri Mwakyembe azindua Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ambayo yanalenga kuonyesha namna mashujaa wa Tanganyika walipambana kupata uhuru, maonyesho ambayo yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja katika Makumbusho ya Taifa- Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam. Uzinduzi wa maonyesho hayo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), kwa lengo ya kuendeleza juhudi za Uhifadhi wa Hifadhi ya Urithi Tanzania,hususani ya Ukombozi wa Afrika yanasimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo, Dkt. Mwakyembe alisema mradi huo wa kuhifadhi historia ya Ukombozi wa bara la Afrika ni muhimu kwa Tanzania kwani unaweza kusaidia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini kuliko ilivyo sasa kwani inawapa nafasi wageni ya kuona mambo tofauti na yaliyozoeleka pindi wanapokuja nchini. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. “Tuna mradi ambao utatupeleka mbali sana Watanzania, Afrika Kusini, Namibia, Angola hata wao wametuambia tusije shangaa sehemu hiyo ikawa inaleta watalii wengi zaidi kuliko wanaokuja kuangalia tembo na simba, urithi wa Afrika tumekabidhiwa na bara la Afrika ni wajibu wetu Watanzania kuusukuma huu mradi maana tumeshachelewa, Watanzania wengi labda hawaelewi mwaka 2011 kwa kushirikiana na UNESCO tulipeleka ombi AU la mradi huu wa bara la Afrika na wakaubariki huu mradi na wakaamua makao makuu yawe Tanzania na sisi tukachagua Dar na hapa kitajengwa kituo kikubwa kitakuwa na historia ya Ukombozi wa Afrika, sisi ndiyo viongozi wa huu mradi,” alisema Dkt. Mwakyembe. Alisema ili kufanikisha mradi huo tayari wameanza kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha pindi watakapojenga kituoambacho kitatumika kuhifadhi vitu mbalimbali ambavyo vilitumika katika kipindi cha ukombozi wa bara la Afrika kuwe na taarifa nyingi kuhusu bara la Afrika. “Tunawatumia wazee walio na historia ya ukombozi wa Afrika tumehoji zaidi ya wazee 100 na tunaendelea na hilo zoezi na tumebaini maeneo zaidi ya 200 Tanzania ambayo yanahitaji kuhifadhiwa, ni wajibu wangu kupeleka muswada bungeni ili tuyahifadhi na kuyalinda kwa kutumia sheria,” alisema Waziri Mwakyembe. Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. Kwa upande wa Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer alisema ni muhimu kwa bara la Afrika kuwa na maonyesho ambayo yanaelezea historia ya bara hilo ili yatumike kuelezea kizazi cha sasa na kijacho namna nchi za Afrika zilipambana kupata uhuru na wao kama EU wataendelea kusaidia miradi mbalimbali yenye lengo ya kutunza urithi wa bara la Afrika. “Ni jambo la kujivunia kwa Umoja wa nchi za Ulaya kusaidia kufanikisha mradi huu … EU tumekuwa tukisaidia miradi mingi na hii yote ni kwa ajili ya kutunza utamaduni na urithi wa bara la Afrika, tumesaidia miradi mbalimbali nchini ikiwepo ya Olduvai na Ngorongoro na tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuendeleza maeneo ya kihistoria,” alisema. Afisa Mpango Kitaifa wa UNESCO, Nancy Kaizilege akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. Naye Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco Dar, Ann Therese Ndong- Jatta katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Mpango Kitaifa wa UNESCO, Nancy Kaizilege alisema ni jambo zuri kuwepo na makumbusho ambayo yanaeleza historia ya bara la Afrika na yatawza kuwapa nafasi watu mbalimbali kutoka mataifa ya nje ya bara la Afrika kuona na kujifunza historia ya Afrika. “Makumbusho haya ni muhimu kwasababu ni sehemu ya ukumbusho wetu kwa baadae, kupitia makumbusho haya tutaona historia ya bara la Afrika, historia ya mwanadamu na safari ya kutafuta uhuru ilivyokuwa,” alisema Kaizilege. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer wakikata utepe katika uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuangalia vitu mbalimbali vya kihistoria ambavyo vimewekwa katikaMaonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.

Monday, October 16, 2017

UHURU FM WALIPOLIAMSHA DUDE JANA KWENYE VIWANJA VYA MWEMBEYANGA, TEMEKE, KATIKA TAMASHA LA 'GUSA MAISHA YAKE' KUMUENZI BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU NYERERE


Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere

Tamasha la Muziki Mnene laacha historia Jijini Mwanza

Binagi Media Group
Maelfu ya wapenzi wa burudani Jijini Mwanza jana wamefurahia tamasha la Mziki Mnene linaloandaliwa na EFM radio na ETV za Jijini Dar es salaa ambapo wasanii mbalimbali akiwemo Kala Jeremiah walipata shangwe kubwa kwenye tamasha hilo lililofanyika uwanja wa CCM Krumba.

Wasanii wengine waliokonga nyoyo za mashabiki zao ni TID, Snura, Young Killer, Baraka Da Prince, Shoro Mwamba pamoja na Msaga Sumu huku Stone Fire akiibuka mkali wa Singeli Michano Mwanza baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 20.

Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika anasema tamasha hilo mbali ya kuwa ni sehemu ya shukurani kwa wasikilizaji wa redio hiyo pamoja na watazamaji wa TVE, pia limelenga kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii hususani wa Singeli.


Tayari limekwisha fanyika katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Mtwara na Mwanza na kwamba litaendelea katika mikoa mingine hivyo mashabiki wa burudani waendelee kufuatilia EFM Radio na TVE kwa taarifa mbalimbali ikiwemo tamasha la Mziki Mnene linalopewa nguvu na Biko pamoja na Cocacola.
Mkali wa Singeli, Msaga Sumu akidondosha burudani kwenye jukwaa la Mziki Mnene CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Saturday, October 14, 2017

ORDINARY TAMUNET MEETINGS


Innocent Nganyagwa Secretary General TaMUNET


John Kitime- President TAMUNET

TANZANIA WOMEN'S BANK YASHIRIKI KIKAMILIFU SIKU YA VICOBA TANZANIA

Banda la TWB au Tanzania Women's Bank lilikuwa moja ya mabanda ambayo yalikuwa mstari wa mbele kuhusu kutoa elimu stahiki kwa watumiaji wa benki hiyo katika siku hii ya Vicoba Tanzania. Vijana wachangamfu waliokuweko katika banda hili walikuwa tayari kutoa elimu yoyote ambayo mtu alitaka kupata kuhusu shughuli ya benki hii ya wote.




Sunday, July 16, 2017

RATIBA YA MSIBA WA MKE WA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO

Mke wa mheshimiwa Waziri wa habari Utamaduni na Michezo, Dr Harrison Mwakyembe, Bi Linah Mwakyembe amefariki usiku wa kuamkia jana Jumapili, katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam alikokuwa anatibiwa. Ratiba ya msiba ni kama ifuatavyo:
Jumanne 18/7/2017 asubuhi mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwa Mhe. Dr Mwakyembe Kunduchi Beach, kisha taratibu za Ibada na kuaga zitafuata na hatimae mwili kusafirishwa kwenda Kyela zitafanyika siku hiyohiyo. Mazishi yatakuwa Kyela siku ya Jumatano
Mungu Amlaze Pema Linnah Mwakyembe

Wednesday, June 21, 2017

MTANDAO WA MUZIKI TAMUNET WAJIPANGA UPYA

Katika kuadhimisha Siku ya Muziki Duniani ambayo husherehekewa kila tarehe 21 June, wajumbe wa Mtandao wa Muziki, Tanzania Musicians Network, leo wamesherehekea kwa kufanya kikao kilichojenga kamati ya uongozi ya mud, viongozi hawa watakuwa katika uongozi kwa mwaka mmoja kisha kutayarisha Mkutano Mkuu wa kuchagua viongozi wa kudumu.  Katika kikao cha leo kilichotumia masaa matatu safu ya uongozi mpya ni kama ifuatayo;
1.  Mwenyekiti - John F Kitime
2.  Makamu Mwenyekiti - Rashid Pembe
3.  Katibu Mkuu - Innocent Nganyagwa
4.  Katibu Mkuu Msaidizi - Geophrey Kumburu
5.  Mweka Hazina - Asha Warsama
6.  Wajumbe - David Ng'asi, Abdul Salvador
TAMUNET ni chama ambacho malengo yake ni kutetea haki za wanachama wake kama wafanyakazi katika tasnia, na kuwa chama rasmi cha wafanyakazi waliomo katika tasnia ya muziki (Musicians Union). Uongozi uliopo unajipanga kuhakikisha chama kinafanya kazi yake ambayo imo katika katiba yake. 
Picha za uongozi mpya wakiwa katika kikao




Friday, April 7, 2017

MWANAMUZIKI UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA FETE DE LA MUSIQUE?


Haya tena wanamuziki wenzangu tamasha la Fête de la Musique linawakaribisha wanamuziki wa kila aina kuomba kushiriki katika msimu wa sita wa tamasha litakalofanyika tarehe 17 mwezi juni 2017 Johannesburg, South Africa. Mwisho wa kupelka maombi ni Ijumaa tarehe 28 April 2017.

Namna ya kuomba

Wasanii wanaotaka kushiriki wapeleke maombi yao yakiambatana na :

·       Maelezo ya historia ya msanii (Artist biography)

·       Picha (Photo)

  • Maelezo ya kiufundi ya vifaa utavyotumia jukwaani (Technical rider)
  • Nakala ya muziki wako (Sound clips)
  • Videos
  • Maelezo yako yatakayoweza kutumika katika matangazo (Press kit)

Maombi yote yanaweza kutumwa kupitia fetedelamusiquejoburg@gmail.com wakati fomu za maombi zinapatikana  HAPA

Fête de la Musique ni tamasha ambalo linaweza kuhudhuriwa na familia nzima bila kujali rika, nia yake ikiwa ni kufurahia muziki wa’live’. Pia ni mahala ambapo wasanii kutoka nchi mbalimbali wanaweza kukutana.

Kwa kuwa kuna maelfu ya wapenzi wa muziki hukutana hapa katika tukio hilo la mara moja kwa mwaka, wanamuziki maarufu na wasio maarufu hupanda jukwaa moja. Tamasha lipo kwa hisani ya Alliance Francaise Johannesburg na French Institute of South Africa, wakishirikiana na Bassline Live kwa ufadhili wa Total.

Mwaka  2016, Fête de la Musique iliwakusanya karibu watu 8 000 katika mji wa Newtown, Johannesburg. Baadhi ya wasanii walioshiriki walikuwa Vaudou Game (France), Blk Jks (South Africa), Les Fantastiques (DRC), Jess & Crabbe (France), Bombshelter Beast (South Africa), Mapumba Cilombo (DRC), Morayks (Lesotho), Zanmari Baré (Reunion Island) na wengine wengi.

Wednesday, March 29, 2017

UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA SANAA UGANDA?


JE,  unataka kushiriki katika tamasha la Bayimba International Festival, ambalo litafanyika tarehe 15-17 September 2017  Kampala, Uganda?

Tamasha la mwaka huu litakuwa ni la kumi. Ni tamasha ambalo linajumuisha muziki, dansa, maonyesho jukwaani, filamu, vichekesho, mashahiri, na sanaa za maonyesho. Wanaohitaji kushiriki ni muhimu kuwa wameshajaza fomu zao na kutuma ifikapo April 30. Katika tamasha la mwaka jana walikuweko wasanii wa Hiphop kama  Akua Naru kutoka Ghana, Tribute ‘Birdie’ Mboweni toka Afrika ya kusini, bibie wa Kiganda ambae ni mpiga saxaphone wa mahadhi ya soul Mo Roots, kundi la Reggae toka Kenya Gravittii Band, na wengine wengi. Kutakuwepo na malipo kidogo kwa washiriki toka nje ya Uganda, japo washiriki wanashauriwa kutafuta njia za kulipia gharama za usafiri, viza na bima mbalimbali. Barua ya utambulisho itatolewa mara utakapokubaliwa kushiriki ili ikusaidie kutafuta ufadhili. Wanaotaka kushiriki wanatakiwa watoe taarifa zifuatazo,

·     Fomu ya ushiriki na kupitia bayimbafestival.com

·     Maelezo mafupi ya wasanii yasiyozidi maneno 800 na picha ya karibuni 

·     Nakala ya kazi yako, kama ni muziki au filamu kazi moja au mbili kwenye CD, DVD or mp3.

·     Mahitaji yako ya vifaa (technical rider/data sheet)

Watayarishaji watawajibu mapema waliofanikiwa.Fomu za maombi zinapatikana pia  HAPA