Thursday, June 19, 2014

COSOTA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA


Rob Hooijer
CHAMA cha Hakimiliki cha Tanzania kimekuwa katika wiki moja na nusu ya warsha, na mikutano ya kukiboresha ambayo inaendeshwa na mtaalamu Robert Hooijer kutoka Afrika ya Kusini. Kazi kubwa iliyokuwa inafanyika ni kuiwezesha COSOTA kufanya kazi katika mifumo ya kisasa ya ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha. Mr Hooijer ni mtu mwenye uzoefu wa miaka mingi katika shughuli za Hakimiliki, aliwahi kuwa CEO wa CISAC, ambacho ndicho muungano wa vyama vyote vya ukusanyaji mirabaha duniani na pia alikuwa CEO wa South African Musicians Rights Organisation (SAMRO) ambayo ndicho chama kikubwa kuliko vyote cha ukusanyaji wa mirabaha Afrika. Kwa kipindi hiki amekuwa Kenya akisaidia shughuli kama hii na mafanikio makubwa yamewezekana huko.









WASANII WAKUTANA NA KUTOA MCHANGO KATIKA UTAYARISHAJI WA SERA YA MILIKIBUNIFU YA TANZANIA



Wasanii kadhaa wakiwemo viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa yote yaliyopo,wiki iliyopita walikutana katika ukumbi wa Chichi Hotel Kinondoni kutoa mchango wao katika utengenezaji wa Sera ya Taifa ya Milikibunifu (National Intellectual Property Policy). Katika mradi huu wa pamoja wa Tanzania Musicians Network (TAMUNET) na Tanzania Film Federation (TAFF), ambao umefadhiliwa na BEST AC, wasanii hawa walipata nafasi kuchangia mambo mbalimbali kuhusu kipengele cha Hakimiliki katika sera ya Milikibunifu. Washiriki wakiongozwa na mtaalamu Ernest Omalla na John Kitime , Mwenyekiti wa TAMUNET na wataalamu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, mambo mengi yalipendekezwa yawemo katika sera hiyo.Bado zinatafutwa taratibu za kuweza kuwapata wadau wengine wa Hakimiliki ili waweze kuongeza ubora wa sera hii.












ARTISTS HOLD A STAKEHOLDERS MEET ON PROPOSED INTELLECTUAL PROPERTY POLICY

The Ministry of Industry and Trade is in the last phase of preparing the National Intellectual Property Policy. The Policy has been in preparation since 2012. A few days ago artists brought together by Tanzania Musicians Network and Tanzania Film Federation with the help of a grant from Best AC, gathered at the Chichi Hotel in Kinondoni and  spent hours coming up with suggestions for the Copyright section of the Policy. Present at the meeting were leaders and members of all the four Federations of Artists and the Tanzania Musicians Network (TAMUNET), also present were officials from the Ministry  of Industry and Trade. Tanzania Musicians Network will work with Tanzania Film Federation in collecting all the suggestions of the artists together with other Copyright stakeholders and together come up with a workable Copyright policy for presentation to the Government.













Wednesday, June 18, 2014

TAMUNET WAFANYA MKUTANO NA WANACHAMA









TAMUNET- Mtandao wa Wanamuziki Tanzania umefanya mkutano katika ofisi za mtandao huo, jirani na Kinondoni Mahakamani, ambao wanamuziki na viongozi wa bendi walialikwa katika kuongelea changamoto zinazoikabili tasnia hiyo. Mkutano huo ulianza kwa Mwenyekiti wa Mtandao John Kitime kutoa ripoti ya utendaji wa Mtandao huo toka ulipoanza na changamoto ambazo Mtandao umepitia.
Baadhi ya mafanikio ya Mtandao huo ni kukamilisha ripoti iliyofadhiliwa na BEST AC ambapo kwa kutumia mtaalamu kutoka Afrika ya Kusini waliweza kutengeneza ripoti iliyoitwa  Study on Artists Copyright Management& Royalties Collection and Distribution in the Tanzania Music Industry. Ripoti hii ilionyesha changamoto za ukusanyaji na ulipaji wa mirabaha kwa wanamuziki wa Tanzania. Nakala ya utafiti huu ilikwisha wasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, ili kuwezesha TBC ambayo ni redio  na TV ya Taifa kuanza kulipa mirabaha kadri ya maelekezo ya sheria ya Hakimiliki na hakishiriki. Bahati mbaya mpaka sasa Wizara haija onyesha ushirikiano kwa hili.
Mtandao pia umeshiriki katika kuwasilisha kwenye Bunge la katiba mapendekezo makuu ya wasanii, i. Wasanii kutajwa  katika Katiba kama kundi maalumu kama walivyotajwa wakulima, wafugaji na wavuvi, kwa kuwa idadi ya wasnii ni kubwa sana, wanaingiza kipato kuliko wavuvi, na inaajiri watu wengi kuliko wavuvi. Pia Mtandao umeluweko katika mchakato wa kutengeneza sera ya Milikibunifu.
Mtandao ni mwananchama wa International Federation of Musicians na mwenyekiti aliwaasa wanamuziki kutumia fursa zinazotokana na uanachama wa shirika hilo.
Kikao kilamua kutengeneza kamati ya kukutana na wanamuziki katika sehemu zao za kazi ili kuongeza wanachama. Na pia kuangalia shughuli za kijamii ambazo wanamuziki wanaweza kufanya kama mchango wao kwa jamii.
Baada ya chakula cha mchana wajumbe walitawanyika