Thursday, October 29, 2015

KATIBU MTENDAJI WA BASATA AMKABIDHI MZEE MAPILI KADI YAKE YA BIMA YA AFYA

Katibu Mtendaji wa BASATA Bwana Ngereza, Mzee Mapili na Mama Shalua mmoja wa maafisa wa BASATA
KUPITIA mpango unaoratibiwa na TAMUNET, ambapo Mtandao huu umeingia makubaliano na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa HHIF, mwanamuziki mkongwe wa siku ntingi ameweza leo kukabidhiwa kadi ya Bima ya Afya. Akikabidhiwa kadi hiyo Mzee Mapili alishukuru Mtandao wa Wanamuziki, na kusema kuwa mpango huu utamsaidia sana kwani ana matatizo ya moyo na figo na anahitaji matibabu na dawa za mara kwa mara. Katibu Mtendaji wa BASATA aliwashauri wanamuziki na wasanii wengine kujiunga na Bima ya Afya

Monday, October 26, 2015

DIAMOND ATWAA TUZO YA MTVEMA


HAKIKA Diamond kiboko yao. TAMUNET inatoa hongera kwa  Diamond Platnumz kwa kushinda MTV European Music Awards (MTVEMA), katika tukio lililofanyika Milan  Jumapili hii tarehe  25 October wakati Tanzania ikipiga kura kutafuta viongozi wake wa miaka mitano ijayo. Tuzo hili hufanyika katika miji mbalimbali ya Ulaya kila mwaka, na washindi huchaguliwa kwa kura za wapenzi kutoka dunia nzima. Mcheza filamu kutoka India na ambae pia alikuwa Miss  World mwaka 2000 Priyanka Chopra pia alishiriki akiwa kundi moja na Diamond, katika ‘ category ‘ ya  Worldwide Act : "Africa/ India". Pamoja na uwingi wa watu wa India , Diamond Platnumz ameweza kupata kura nyingi zaidi na kuongeza sifa wake mwenyewe binafsi na kwa Taifa. Hongera tena Diamond
Priyanka Chopra

Saturday, October 24, 2015

Profesa Elisante Ole Gabriel ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali. Kati Makatibu Wakuu hao Rais amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, kuwa Katibu Mkuu na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga kuhamishiwa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari. Hakika hii ni habari nzuri kwa wasanii katika kipindi hiki tunapongojea matokeo ya uchaguzi Mkuu. Profesa ni mchapa kazi wa ukweli, ni kati ya mambo mazuri makubwa yaliyotokea katika Wizara hii kwa muda mrefu

Wednesday, October 21, 2015

DOUBLE M WAKO MSUMBIJI KWA MARA YA PILI



Baada ya kazi nzuri ya awali Double M Sound chini ya Muumin Mwinyjuma imealikwa tena Msumbiji. Kwa maneno yake mwenyewe kiongozi huyu wa kundi hilo alituma ujumbe huu, “Nipo  njiani na vijana wangu tunaenda Msumbiji, tumepata mualiko  mwingine, safari hii tumealikwa na serikali kupitia Manispaa ya Mkoa Wa PEMBA, baada ya kufurahishwa na kazi yetu ya mwezi uliopita. Kuna sherehe ya Kitaifa ambayo hua inazunguka kila Mkoa na mwezi huu inafanyika ktk Mkoa Wa Mpemba, kutakua na burudani za aina nyingi  tofauti. Safari Hii tumetakiwa kuwa na idadi ya watu 14 tofauti na safari ya kwanza tulikwenda 19.
Kwenye msafara wetu tupo watu 13 na mwenzetu mmoja fundi mitambo na mpiga tumba Omar Zagalo alibaki kule na vyombo toka tulipoenda mara ya kwanza. Tulio kwenye msafara huu ni mimi Muumin Mwinyjuma, Rashid Sumuni-solo, Pascal Kinuka-bass, Issa Ramadhani-kinanda, H Waninga-drums, Amina Juma, Salehe Kupaza na  Dogo Rama waimbaji, madansa ni Verosa,Regina, Salma, Titi na Star. Tunasafiri kwa njia ya bus tukishavuka Boda saa 10 Jioni tutachukuliwa na gari lililoandaliwa na wenyeji wetu, ambayo itatumia saa 1-30 kutufikisha mji wa Msimbwe na hapo tutapanda ndege maalum itakayotupeleka Pemba. Tuombeeni Mungu tufanye vizuri zaidi kwani Show hii ni muhimu sana kujitangaza na kuutangaza muziki wa Bendi za TZ."

Tuesday, October 20, 2015

MSONDO NGOMA WAKUBALIANA KUPATA BIMA YA AFYA.

KATIKA  mkutano uliofanyika leo kwenye makao makuu ya MSONDO, wanamuziki waliweza kupata taarifa ya namna BIMA YA AFYA inavyofanya kazi. Maelezo hayo yaliyotolewa kwao na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki, (TAMUNET) John Kitime. Baada ya mkutano huo wanamuziki hao walikubaliana kuanza kuhakikisha kila mmoja wao ana Bima ya Afya mara moja


Sunday, October 11, 2015

DIAMOND AZOA TUZO TATU AFRIMMA AWARDS


diaDiamond Vannessa Mdee na Ommy Dimpoz wameweka historia kwa maisha yao, nay a muziki wa Tanzania kwa kushinda Tuzo katika Afrimma Awards 2015, zilizofanyika Dallas Marekani leo. Diamond akiwa ameshinda tuzo 3 zikiwemo Best Dance Video- Nana, Best Male Artists East Africa, na Artiste of the Year Vannesa Mdee akachukua Tuzo ya Best Female Artists East Africa. Ommy Dimpoz akishinda tuzo ya Best Newcomer> Diamond amkuwa katika tuzo jingine kutokana na wimbo alioshirikiana na Mnaijeria Tiwa Savege, hivyo kupata tuzo ya Best Inspiration Song Hongera kwa wote Best Male – East Africa
  • Eddy Kenzo (Uganda)
  • Jaguar (Kenya)
  • Diamond Platnumz (Tanzania)
  • Bebe Cool (Uganda)
  • Jackie Gosse (Ethiopia)
  • Ali Kiba (Tanzania)
  • Dynamq (Sudan)
Best Female – East Africa
  • Khadija Kopa (Tanzania)
  • Aster Aweke (Ethiopia)
  • Victoria Kimani (Kenya)
  • Vanessa Mdee (Tanzania)
  • Juliana Kanyamozi (Uganda)
  • STL (Kenya)
  • Irene Ntale (Uganda)
vannessa

 Best Newcomer
  • Kiss Daniel (Nigeria)
  • Pappy Kojo (Ghana)
  • Korede Bello (Nigeria)
  • Lil Kesh (Nigeria)
  • Mz Vee (Ghana)
  • Fabregas (Congo)
  • Ommy Dimpoz (Tanzania)
  • Bebi Philip (Ivory Coast)
  • mpata Wapi’ (Tanzania)
  • Sauti Sol – ‘Sura Yako’ (Kenya)
  • Cassper Nyovest – ‘Doc Shabaleza’ (South Africa)
  • ommy
Artist of the Year
  • Flavour (Nigeria)
  • Diamond Platnumz (Tanzania)
  • Sarkodie (Ghana)
  • Cassper Nyovest (South Africa)
  • Davido (Nigeria)
  • Fally Ipupa (Congo)
  • Eddy Kenzo (Uganda)
  • Wizkid (Nigeria)
  • Yemi Alade (Nigeria)
  • Bucie (South Africa)
Inspirational Song
  • Bracket ft. Diamond & Tiwa Savage – ‘Alive’ (Nigeria & Tanzania)
  • Irene Ntale – ‘Woman’ (Uganda)
  • Sarkodie ft. Castro – ‘Adonai’ (Ghana)
  • Jose Chameleon – ‘Bwerere’ (Uganda)
  • Psquare ft. Dave Scott – ‘Bring it On’ (Nigeria)
  • Eddy Kenzo – ‘Be Happy’ (Uganda)
 

Thursday, October 8, 2015

TAMUNET YAFANYA MKUTANO

Wa kwanza kushoto, Abraham Kapinga (Tanzanite Band) Katibu Mkuu wa Mtandao

Toka kushoto-Innocent Nganyagwa, Ally Jamwaka(Sikinde), Rashid Pembe(Mark Band), Davidi Ng'asi(Mwalimu wa muziki)

Abdul Salvador
Wanamuziki kadhaa walikusanyika jana kwenye ofisi za TAMUNET, Tanzania Musicians Network kujadili mambo kadhaa yanayohusu wanachama wa Mtandao huo. Baadhi ya mambo yalitojadiliwa ni tathmini ya wanamuziki kujiunga na Bima ya Afya, Tamasha la sanaa litakalokuweko March 2016 huko Ivory Coast, ushiriki wa Mtandao katika uboreshaji wa elimu ya muziki, na pia kuangalia nafasi ya maendeleo ya muziki katika serikali ijayo.
Ilionekana kuwa kasi ya kujiunga na bima ya afya bado ni ndogo, na moja ya sababu ni ukosefu wa uelewa kuhusu umuhimu wa Bima na namna ya utendaji wa Bima. Mikakati ilipangwa kukabili hali hiyo.
Taaarifa ya Tamasha ilikwisha anza kusambazwa kutumia mitandao ya Facebook, vikundi vya Whatsapp Blog hii na taarifa za mdomo. Tayari wasanii kadhaa walionyesha nia ya kushiriki. Mtandao uangalie namna ya kwezesha wanamuziki hawa kufanikiwa katika ushiriki wa tamasha hili.
Ilikuablika kuwa katika wiki mbili zijazo kufanyike kikao cha kuangalia utekelezaji wa kushiriki katika kuboresha elimu ya muziki. Mwanamuziki na Mwalimu wa Muziki David Ng'asi alipewa jukumu la kuja na andiko la awali la mkakati huo.

Monday, October 5, 2015

MWALIKO WA KUSHIRIKI TAMASHA LA 9 LA MASA -IVORY COAST

WANACHAMA  wa Tanzania Musicians Network (TAMUNET) mnakaribishwa kushiriki katika tamasha la 9 la MASA litakalokuwa Abidjan Ivory Coast kati ya tarehe 5-12 March 2016. Kwa maelezo zaidi wasiliana uongozi kupitia 0713274747 au 0763722557. Au wasiliana kupitia musicnettz@gmail.com