Saturday, November 26, 2016

CDEA WAZINDUA MRADI WA ATAMISHI YA KAZI ZA SANAA ‘IIDEA’ KUSAIDIA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA) leo limezindua rasmi mradi wa Atamishi ya kazi za sanaa (IIDEA) ambapo utakuwa nguzo muhimu kwa nchi za Umoja Wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye, ameeleza kuwa sanaa ni ajira hivyo mpango huo utasaidia kuinua ajira kwa wasanii watakaofikiwa na kukuza soko la Afrika Mashariki kupitia Sanaa zao.
“Sanaa ni kazi ya kujikimu na kazi ni hutu hivyo ni wajibu wa kila msanii kujiheshimu na kufuata taratibu ili kuwa njia kwa jamii na kuheshimika zaidi hasa katika sanaa yake. Nawapongeza sana CDEA kwa mpango huu kwani utaendelea kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, utasaidia Wasanii wetu kupanua mawazo yao zaidi na kujiongezea maarifa ya juu katika taaluma yao ya Sanaa.” Alieleza Bw. Habibu Msammy.
Pia alisisitiza kuwa mafunzo watakayoyapata wayatumie kujiimalisha kiuchumi huku akisisitiza kuwa bado wanayo nafasi ya kujifunza zaidi katika kuweza kubuni vazi la Taifa.
“Kwa kuwa mradi huu unagusa sanaa za Ubunifu wa mavazi, Urembo na filamu. Wabunifu wa Tanzania ni wasaha wa kuendelea kubuni vazi la Taifa, Wasanii wanaangaliwa na wengi hivyo kuanzia mavazi na mawazo yao ya ubunifu na tunawategemea pia katika kubuni vazi letu la Taifa” alieleza Habibu Msammy.
Mradi huo wa mwaka mmoja unatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa wabunifu wa mavazi na urembo, Wanamuziki na wasanii wa filamu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa amebainisha kuwa, baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa wataanza mchakato wa kupata washiriki ambapo wahusika watatakiwa kutuma maombi ya ushiriki baada ya kuona matangazo mbalimbali yatakayotolewa na CDEA kupitia mitandao ya kijamii na sehemu zingine za Utamaduni.
Katika uzinduzi huo, watu mbalimbali wameshiriki wakiwemo wasanii wa filamu, maigizo, wabunifu wa mavazi, wanahabari, wanamuziki na wasanii wa kazi za sanaa ikiwemo za mikono na ubunifu.
dsc_1296
Afisa wa Mradi wa IIDEA, Bi. Angela Kilusungu wa CDEA, akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo mpya wa utakaosaidia sanaa kwa Afrika Mashariki
dsc_1306
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya CDEA, wakiwa katika mkutano huo
dsc_1316 dsc_1333
Allen Enjewele wa CDEA akifanya mahojiano katika tukio hilo
dsc_1354
Msanii Remigius Sostenes wa CDEA akitoa burudani katika tukio hilo
dsc_1337
Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akijadiliana jambo na Mjumbe wa bodi hiyo ambaye anatokea Burundi, Bw. Gilbert Hagabimana wakati wa uzinduzo huo.
dsc_1341
Baadhi ya wadau wa Sanaa nchini wakijadiliana katika uzinduzi huo
dsc_1342 dsc_1346
Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa (kushoto) akijadiliana jambo na wadau wa sanaa
dsc_1348 dsc_1357
Msanii Nick wa Pili akielezea namna sanaa inavyohitaji ubunifu wakati wa tukio hilo
dsc_1369
Baadhi ya wadau wa sanaa na wanahabari wakipata kujadiliana jambo
dsc_1406
Wadau wa sanaa wakifuatilia makala fupi ya CDEA iliyokuwa maalum wakati wa uzinduzi huo
dsc_1408
Uzinduzi huo ukiendelea
dsc_1427
Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa akielezea jambo katika tukio hilo
dsc_1433
Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akitoa neno na kumkaribisha mgeni rasmi
dsc_1440
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua rasmi mradi huo
dsc_1434
Mzee Kitime mmoja wa wadau wa Sanaa nchini akifuatilia kwa makini tukio hilo la uzinduzi
dsc_1438
Wadau wa kifuatilia uzinduzi huo
dsc_1455 dsc_1461
dsc_1471
cdea
Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya uzinduzi wa mradi huo wa IIDEA, mapema leo Novemba 25.2016.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE

Tuesday, November 22, 2016

Mkataba wa Kumkodi Mwanamuziki au Mwimbaji Msindikizaji Kwa ajili ya kurekodi

Ni jambo la kawaida kabisa kuona makubaliano makubwa katika tasnia ya muziki Tanzania yanafanywa bila mikataba bali kwa makubaliano ya mdomo. Hili ni tatizo ambalo lazima lirekebishwe, kwani linaleta hasara kubwa kwa wasanii kutokupata haki zao stahili na mara nyingine kudhulumiwa kabisa. Hivyo basi kwa kuwa mikataba ya muziki huwa na lugha ngumu ifuatayo ni mikataba mabayo imerahisishwa na UNESCO ili wanamuziki waweze kuitumia kwa marekibisho kidogo kutegemeana na hali halisi. Hii ni mifano ya mikataba ambayo hutumika dunia nzima. Usikubali kuanza kazi bila mkataba wa maandishi…. JE UNATAKIWA KUFANYA KAZI YA MUZIKI KWENYE ALBUM YA MTU MWINGINE? MKATABA HUU HAPA  
 
 Mkataba wa kumkodi Mwanamuziki au Mwimbaji Msindikizaji Kwa ajili ya kurekodi Santuri 

 Mkataba unaeleza masharti ya kumkodi mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji kwa ajili ya kurekodi santuri moja au zaidi zitakazotayarishwa kibiashara. Mkataba unaainisha wajibu wa mtayarishaji na vilevile ule wa wanamuziki na waimbaji.

 MWANAMUZIKI AU MWIMBAJI MSINDIKIZAJI MTAYARISHAJI WA SANTURI 
 KIFUNGU CHA 1 – Madhumuni.  
Mtayarishaji anamkodi mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji katika nafasi yake ya kitaalamu kurekodi santuri moja au kadhaa. Santuri zitatumiwa mojamoja au kama sehemu ya Albamu. Mkataba lazima ujazwe kikamilifu pale inapobidi, kwa kuzigatia masharti ya sheria za kazi za nchi ambazo mkataba unasainiwa. 
 KIFUNGU CHA 2 – uidhinishaji wa Matumizi. MWANAMUZIKi au MWIMBAJI MSINDIKIZAJI anaidhinisha upangiliaji wa maonesho yake na kurudufu santuri zilizoainishwa kwenye kifungu cha 1 na vile vile kufanya biashara ya santuri hizo kwa umma. Hivyo mtayarishaji atakuwa na haki ya kuzalisha, kuchapisha, kusambaza itakuvyokuwa kuuza kwenye kibebeo cha aina yoyote ( K7, CD, DVD ya sauti au muundo wowote wa siku zijazo nk ) au kwa mawasiliano ya mtandao (Intaneti na mingineyo), kutangaza katika muundo wowote, chini ya kichwa cha habari, nembo au alama ya chaguo lake na duniani kote, santuri zilizoanishwa katika kifungu cha 1. Unufaikaji wowote zaidi ya matumizi yaliyoelezwa hapo juu, yakiwamo matumizi kwa ajili ya matangazo ya biashara, matumizi ya kielimu, matumizi katika sinema au onesho, na matumizi kwenye bidhaa maalumu, yatahitaji kwanza kupata idhini ya asasi ya usimamizi wa pamoja inayosimamia haki za wanamuziki na waimbaji wasindikizaji. Ili kuruhusu matumizi sahihi ya haki. Mtayarishaji anawajibika kuhakikisha mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji anasaini karatasi ya kurekodi kipindi kulingana na taratibu za kitaalamu, na kuwasilisha nakala ya karatasi hii ya kurekodi kipindi kwenye asasi ya usimamizi wa pamoja ambayo inasimamia haki za wanamuziki na waimbaji wasindikizaji katika nchi zilizotarishwa santuri. Zaidi ya hayo msanii anaridhia matumizi ya jina na picha yake, kama vitahitajika, kuhusiana na matumizi ya santuri hizo. 
 KIFUNGU CHA 3 – Wajibu wa mtayarishaji. MTAYARISHAJI anajukumu la kuheshimu wajibu wote uliowekwa na sheria za kijamii kuhusiana na kumkodi MWANAMUZIKI au MWIMBAJI MSINDIKIZAJI. Mtayarishaji anawajibika kumlipa mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji kiasi cha _____________________ kwa kila kipindi cha kurekodi, ili kufidia kushiriki kwake katika kurekodi santuri, na vilevile kwa ajili ya uchapishaji na mauzo ya miziki kwenye aina yoyote ya kibebeo (K7, CD, DVD ya sauti n.k) au katika mawasiliano ya mitandao (Intaneti au mingineyo). Upigaji wa santuri katika utangazaji utatakiwa kuliipiwa moja kwa moja na mashirika ya utangazaji kwenye asasi ya usimamizi wa pamoja ambayo inasimamia haki za wanamuziki na waimbaji wasindikizaji katika nchi matangazo yanamotolewa. 
 KIFUNGU CHA 4 – wajibu wa Mwanamuziki au Mwimbaji Msindikizaji. 
Mwanamuziki kutoka nje au mwimbaji msindikizaji kutoka nje ya nchi anahakikisha kuwa amepewa kibali cha kufanya kazi kwenye nchi santuri zinapotayarishwa na kuwasilisha uthibitisho wa jambo hilo. Mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji anawajibika kuwepo kuanzia ___________________ hadi
___________________katika sehemu ifuatayo _____________________ kushiliki katika vipindi vya kurekodi ambavyo vitafanyika kulingana na ratiba zifuatazo:- ______________________________________________________________________________ Kifungu cha 5 – mambo mbalimbali  
Mkataba huu unaongozwa na sheria ya nchi unamofanyika utayarishaji. 
Umesainiwa (mji)…………………………………….. Tarehe ……………….. Katika ……………… nakala halisi. 
 MWANAMUZIKI AU MWIMBAJI MSINDIKIZAJI ________________________________________________________________________   MTAYARISHAJI ________________________________________________________________________  

Tuesday, November 8, 2016

PUMZIKA KWA AMANI SAMWEL JOHN SITTA

Mzee Samwel John Sitta alikuwa rafiki mkubwa wa wasanii na jambo ambalo wengi hawalijui ni kuwa pia alikuwa msanii mpiga gitaa. Mwalimu wa Mzee Sitta ambaye nae ni marehemu Mzee Brown Swebe aliwahi kusema kuwa alimfundisha gitaa Mzee Samweli Sitta wakati yuko shule ya sekondari Tabora, na alifanya hivyo kwa malipo ya kulima matuta kadhaa ya viazi. Wakati wote alikuwa kigusia umuhimu wa Hakimiliki na hata wakati akiwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba aliwezesha wasanii kukutana na wajumbe wengi wa Bunge la katiba kuweza kujielezea kuhusu umuhimu wa ulinzi wa mali isiyoshikika kutajwa katika katiba.





Tutakukumbuka daima Mzee Samwel  John Sitta