Wednesday, October 30, 2013

WANAMUZIKI WA TANZANIA WAFANYA WARSHA KUBWA







Martin Cuff

 Warsha kubwa ya siku moja ya wanamuziki wa tanzania yafanyika pale Nyumbani Lounge. Wanamuziki kutoka kila aina ya muziki walikuweko. katika warsha hii iliyoomgozwa na mtafiti Martin Cuff ilikuwa ni kutoa report ya utafiti wake kuhusu hali halisi ya utekelezaji wa Ukusanyaji na ugawaji wa Mirabaha. Wanamuziki walipata nafasi ya kuchangia  na kutoa mapendekezo. Ripoti nzima kutoka katika wiki mbili zijazo. Utafiti ulifanywa na Martin Cuff na kuongozwa na Tanzania Musicians Network kwa ufadhili wa BEST AC.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya habari Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel ndie aliyefunga warsha hii kwa kusifu jitihada hii ya wanamuziki kufanya utafiti. Katika kukutana huku na Naibu Katibu mkuu wanamuziki walioingia mkataba na kampuni mojawapoya ringtones walilalamika kuwa waliingia mkataba wa miaka kumi na kampuni hiyo na baada ya hapo kampuni hiyo haikutaka hata kujibu barua zao, Naibu Katibu Mkuu aliwaita wahsanii hao ofisini kwake ili kuona cha kufanya, pia alimtaka Mwenyekiti wa Tanzania Musicians Network John Kitime amuone ili waongelee tatizo la TBC kutokulipa mirabaha na kuatafuta suluhu.


















Monday, October 28, 2013

MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA WAFANYA WARSHA YA SIKU MOJA


 
WANAMUZIKI takriban 70 leo wameshinda siku nzima wakijadili ripoti ya utekelezaji wa Hakimiliki katika kipengele cha kukusanya na kugawa mirabaha. Wanamuziki wakiongozwa na mtafiti kutoka Afrika ya Kusin martin Cuff leo walifanya warsha hiyo katika ukumbi wa Nyumbani Lounge. Warsha ilifungwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya habari, Utamaduni na Michezo aliyesifu jitihada za wanamuziki kuweza kufanya kikao kama hiki.

Sunday, October 20, 2013

PRODUCERS WAHUDHURIA SEMINA YA HAKIMILIKI

Pamoja na kuwa leo ni siku ya Jumapili, watu wengi huwa wanapumzika, maproducer kadhaa wamejikusanya na kuhudhuria semina ya Hakimiliki iliyoendeshwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki John Kitime. Semina hiyo iliyofanyika katika jengo la Sayansi na Teknolojia iliwawezesha Producers kufahamu nini maana ya Hakimiliki na vilevile kupata elimu ya awali kuhusu yaliyomo katika sheria ya Hakimiliki ya hapa nchini

JULIUS NYAISANGAH.... UNCLE J.,,.SUPER TALL HATUNAE TENA

MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA UNATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA NDUGU , RAFIKI, NA WANAMUZIKI WALIOWAHI KUFANYA KAZI NA MTANGAZAJI MKONGWE JULIUS NYAISANGA, ALIYEFARIKI USIKU WA KUAMKIA LEO 20 OKTOBA, 2013 KATIKA HOSPITALI YA MAZIMBU MOROGORO.
MUNGU AMLAZE PEMA JULIUS, KAZI YAKO ULIOIFANYA KATIKA TASNIA YA MUZIKI HAITAFUTIKA

Wednesday, October 16, 2013

Je unapenda muziki wa Mashujaa Band?

Bendi ya Mashujaa imetengeneza ukurasa wao ambapo unaweza sasa kusikiliza nyimbo zao nyingi kutoka hapo. Je wewe au bendi yako mnanyimbo katika mtandao wa intanet, basi tutumie anwani au wimbo kupitia musicnettz@gmail.com ili tuuweke katika blog yetu.
Kwa kusikiliza nyimbo za Mashujaa ingia HAPA upate nyimbo zao

Thursday, October 3, 2013

KIPINDI CHA MIKIKI MIKIKI YA MUZIKI KUANZA KURUKA JUMAMOSI HII SAA 12:30 JIONI TBC RADIO YA TAIFA

BAADA ya kupata ufadhili wa BEST AC kwa kupitia Tanzania Heritage Project, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TMN), utaanza kurusha vipindi vya radio kupitia Radio TBC Taifa. Vipindi hivyo ambavyo vitaendeshwa na mwanamuziki na mwenyekiti wa Mtandao John Kitime. Kipindi cha kwanza kitaanza na kuangalia biashara ya muziki kwa kutegemea viingilio ilivyo na kama kweli inalipa na kitashirikisha kwa kukusanya maoni kutoka kwa wasikilizaji. Kipindi hiki ni mwanzo wa vipindi vingi vya redio vitakavyohusu muziki kama utamaduni, taaluma na kama biashara. Karibuni tusikilize na tutoe maoni kupitia blog hii na ukurasa wa facebook  https://www.facebook.com/wanamuzikiwa.tanzania Wanamuziki wa Tanzania tuna uwezo kama wanamuziki wengine duniani lakini tuna matatizo makubwa ya mpangilio katika tasnia yetu