Thursday, July 10, 2014

MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA, AFUNDISHA WAALIMU WA NURSERY MUZIKI

Ili kupata kizazi kitakachoweza kupenda muziki na kutumia vifaa vya muziki ni vizuri kuhakikisha unapata waalimu bora wa muziki. Na ni vizuri kuanza kufundisha watoto wakati wakiwa bado wadogo. Kufanikisha hili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania-John Kitime, akishirikiana na Chuo cha Montesori cha Waalimu wa Shule za Nursery, wameanza mpango wa kuwawezesha waalimu kujifunza japo chombo kimoja cha muziki, na pia njia rahisi za kutunga nyimbo za watoto. Waalimu wanafunzi watarekodi nyimbo walizotayarisha na kuondoka nazo baada ya kumaliza masomo ili waweze kuzitumia kufundishia wanafunzi kwenye vituo vyao.