Monday, September 30, 2013

WANAMUZIKI WAWILI WA TEMEKE WAFARIKI LEO

Msanii wa kundi la WATEULE, Malik Ahmed Moa maarufu kwa jina la Mack2B amefariki dunia leo. Msiba utakuwa Yombo kwa wazazi wake Mack 2B alikuwa producer na msanii wa raga, amefariki kutokana na ugonjwa wa figo uliokuwa unamsumbua muda mrefu
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMIN

**********************************************************
Joseph akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wakati akiwa African Stars
Mwanamuziki mpiga bezi wa siku nyingi Joseph Watuguru
amefariki mchana huu katika hospitali ya Amana. Watuguru amewahi kupigia bendi nyingi zikiwemo Bantu Group ya Hamza Kalala, Magoma Moto Sound, African Stars ile ya mwanzo kabisa Mchinga Sound, na katika siku zake za mwisho alikuwa bendi ya WK Sound ya Temeke. Watuguru aliwahi kushiriki katika bendi iliyotengenezwa na Producer kutoka Norway Sigbjorn Nedland iliyoitwa Mradi Group akiwa na akina Bob Rudala, Keppy Kiombile, John Saggati, Bizimana Ntavyu, Anania Ngoliga na wengine. Alikuwa mpiga bezi mzuri na pia fundi mitambo wa kutegemewa
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMINA

Tuesday, September 17, 2013

MTANDAO KUANDAA SEMINA YA WANAMUZIKI KUHUSU UKUSANYAJI NA UGAWAJI WA MIRABAHA KATIKA KAZI ZA MUZIKI

Kamati ya kuratibu mradi unaoendelea wawa Utafiti wa hali halisi ya ukusanyaji na ulipaji wa mirabaha leo imekaa na kupanga kufanya semina ya awali kwa baadhi ya wanamuziki ili kuanza kuelimisha taratibu za ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha. Semina hiyo itafanyika katika muda wa wiki mbili. Semina itahusisha wanamuziki wa aina tofauti za muziki, dansi, taarab, bongoflava, hiphop, gospel muziki asili nakadhalika

Sunday, September 15, 2013

MTANDAO WA MUZIKI TANZANIA WAPATA UFADHILI WA BEST AC


MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA umepata ufadhili kutoka Business Environment Strengthening of Tanzania (BEST – AC) ili kuweza kufanya utafiti wa kina kupata ukweli wa hali halisi ya ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha ya muziki unaofanywa na COSOTA, na baada ya hapo kutoa ushauri wa nini kifanyike ili kuboresha hali iliyopo. Madhumuni ya mradi huu ni kuwezesha kufanya mabadiliko katika tasnia ya muziki ambayo yatatengeneza nafasi za ajira zenye tija ili kuwezesha tasnia kutoa mchango wake katika pato la Taifa, na kukuza sifa ya nchi kutokana na wasanii wengi wenye sifa waliomo hapa nchini.

Mradi utaangalia sheria zilizopo zinazohusu ugawaji wa mirabaha ya wanamuziki na mambo mengine yote yanayohusiana na shughuli ya ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha na kupendekeza taratibu za kuboresha hali.

Kamati za fedha na utawala zitaanza kazi wiki hii ili kuweza kufanikisha zoezi hili ambalo linatakiwa likamilike katika muda wa mwezi mmoja. Wanamuziki watashirikishwa katika semina ambayo itafanyika katika wiki chache zijazo.  Mtafiti kutoka Afrika ya Kusini amekwisha ingia mkataba na Mtandao ili kufanya kazi hiyo.

TANZANIA MUSICIANS NETWORK SECURES A GRANT FROM BEST AC



TMN has secured a grant from Business Environment Strengthening of Tanzania (BEST – AC) to conduct a study to assess the existing arrangement under COSOTA in collection of music royalties and use the findings to provide clear and precise recommendations for appropriate interventions to advocate for change in collection system for the music industry growth of Tanzania.
The objective of the project is to initiate appropriate interventions that will support the Tanzania music industry to create the much needed jobs, subsequently taxes flowing back to government and enhancing the image of country built up from the talented artistes from institutionalized support for the industry.
The Project will specifically carry out a study to assess the legal framework regulating the distribution of royalties to musicians and other owners of copyright in works and all matters connected thereto and provide a report with recommendations.  The report will be used to engage with government to address the inefficiencies established with a purpose to strengthen the musicians' bargaining power in controlling the usage of their copyright.
The project is aims to examine the music industry landscape and the struggle on copyright protection, combating piracy, legislative instruments to implement copyright and managing music rights; mandate, transparency, fairness in collection and timely payment of royalties to artists.  The purpose is to seek government’s support to have clear distinguished roles of the Copyright Society of Tanzania (COSOTA) as a Government copyright office from that of collecting organization. The project should identify the important stake holders in the industry such as Publishers, Distributors, Manufacturers of musical works, lyrists, arrangers, producers, executive producers and such others and their roles in the Royalties payment chain.

Tuesday, September 3, 2013

MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAMUZIKI JOHN KITIME, ATEULIWA MJUMBE WA BASATA


Profesa Penina Mlama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Penina Mlama kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari - MAELEZO leo, Uteuzi huo wa Profesa Mlama unaanzia mwaka 2013 na unatarajia kumalizika mwaka 2016.
Prof. Mlama ni Profesa wa Sanaa na Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aidha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ameteua jumla watu 12 kuwa wajumbe wa BASATA kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka huu.
Walioteuliwa ni pamoja na wawakilishi wa Vyama na Asasi mbalimbali wa Baraza hilo ambao ni Dkt. Vincensia Shule, John Kitime , Angela Ngowi, Dkt. Herbert Makoye, Erick Shigongo na Alex Msama.
John Kitime

Wawakilishi wengine ni pamoja na Juma Adam Bakari, Daniel Ndagala, Michael Kadinde na Joyce Fisoo.
Wanaoingia kwa mujibu wa nyadhifa zao ni Prof. Hermas Mwansoko na Katibu Mtendaji wa BASATA.
Katika hatua nyingine Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua Bwana Ghonche Materego kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Kabla ya uteuzi huo Materego alikuwa amemaliza muda wake kama Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa.
Wajumbe wa Bodi hiyo walioteuliwa na Waziri Mukangara ni Dkt. Herbert Makoye, Prof. Emanuel Mbogo, Dkt. Lucy Mboma, Prof. Hermas Mwansoko pamoja na Katibu Mtendaji wa BASATA.
Wakati huo huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ameteua jumla ya watu 21 kuwa wajumbe wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.
Wajumbe hao ni Dkt. Shani Omari, Prof. Yohana Msangila, Ester Riwa, Dkt. Issa Zidi, Khadija Juma na Dkt. Martha Qorro.
Wengine ni Mmanga Mjawiri, Razia Yahaya, Richard Mbaruku, Selina Lyimo, Keneth Konga, Amour Khamis, John Kiango, na Shani Kitogo.
Wajumbe wengine ni Ally Kasinge, Ahmed Mzee, Rose Lukindo, Shabani Kisu pamoja na Edwin Mgendera.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo la BAKITA atachaguliwa na wajumbe watakapokutana kwenye kikao chao cha kwanza.