![]() |
| KIONGOZI WA BENDI |
Wednesday, July 31, 2013
MWENYEKITI NA MWEKA HAZINA WA TANZANIA MUSICIANS NETWORK WAKITIA SAINI MAKUBALIANO YA UTAFITI KUHUSU HALI YA MUZIKI TANZANIA
BEST AC imeuwezesha Mtandao wa muziki Tanzania kufanya utafiti wa kina na kisha kuja na majibu ya matatizo ya wanamuziki wa Tanzania hasa katika swala la Hakimiliki. Katika makubaliano hayo Mtandao utapata dola 49,000, zitakazolazimika kupatikana kwa ripoti katika muda wa miezi mitatu ijayo
![]() |
| Hans muwakilishi wa BEST AC |
![]() |
| Mwenyekiti wa Mtandao John Kitime akitia sahihi makubaliano hayo kwa niaba ya Mtandao |
![]() |
| Asha Warsama Salvador Mweka hazina akitia sahihi kwa niaba ya Mtandao |
KIKAO CHA MUHIMU CHA WANAMUZIKI CHAFANYIKA BASATA LEO
Wanamuziki chini ya chombo chao kipya Tanzania Musicians Network (Mtandao wa Wanamuziki Tanzania) leo wamekutana katika ukumbi wa BASATA na kufanya mkutano amba katika mkutano huo wameongelea mambo muhimu yafuatayo;
Pamoja na maelezo hayo wanamuziki walitaarifiwa kuwa Mtandao umepata ofisi katika maeneo ya Kinondoni jirani na American Chips katika mtaa yalipo Makao Makuu ya CHADEMA. Kodi ya ofisi imekwisha lipia na baadhi ya samani zimenunuliwa, japo wanamuziki waliombwa kama wana samani yoyote wanayoweza kujitolea itapokelewa kwa mikono miwili.
Wanamuziki walitaarifiwa kuwa kupatikana kwa ofisi kutarahisisha uandikishaji wa wanachama wapya. Malipo ya wanachama yapo kama ifuatavyo.
Fomu za uanachama- 1000/-
Kiingilio - 20,000/-
Ada -5,000/- kwa mwaka, fomu zitaanza kupatikana JUmatatu ijayo katika ofisi mpya ya chama.
Wanachama walitaarifiwa kuwa anwani ya email ya cham ni musicnettz@gmail.com na blog hii ilitambulishwa. Wanamuziki waliombwa kuitumia blog hii kama gazeti lao la kuelezea shughuli zao zote bila kuwa na woga.
Tuesday, July 30, 2013
MKUTANO WA WANAMUZIKI WOTE BASATA
Mkutano wa wanamuziki kuweko Jumatano tarehe 31 July 2013, BASATA, kuanzia saa nne hadi saa sita. Katika mkutano huo ajenda kubwa itakuwa kutambulisha Mtandao upya kwa wanamuziki na kupeabna taarifa za hali halisi, na kisha kupeana majukumu, wanamuziki wa kila aina aina ya muziki tunakaribishwa.
Thursday, July 25, 2013
MWANAMUZIKI WA ZIMBABWE CHIWONISO MARAILE AFARIKI DUNIA
Mwanamuziki Chiwoniso Maraile wa Zimbabwe amefariki dunia baada ya kuugua kwa matatizo ya mapafu. Chiwoniso ambaye amewahi kuja Tanzania na kurekodi katika studio za Marimba Studio akifanya kazi na wanamuziki wa hapa nchini kama Karola Kinasha, Norma Bikaka, Bob Rudala, alikuwa mahiri sana kwa chombo chake cha Mbira na kuimba pia.Mungu amlaze pema mwenzetu
Subscribe to:
Comments (Atom)






