Wednesday, June 21, 2017

MTANDAO WA MUZIKI TAMUNET WAJIPANGA UPYA

Katika kuadhimisha Siku ya Muziki Duniani ambayo husherehekewa kila tarehe 21 June, wajumbe wa Mtandao wa Muziki, Tanzania Musicians Network, leo wamesherehekea kwa kufanya kikao kilichojenga kamati ya uongozi ya mud, viongozi hawa watakuwa katika uongozi kwa mwaka mmoja kisha kutayarisha Mkutano Mkuu wa kuchagua viongozi wa kudumu.  Katika kikao cha leo kilichotumia masaa matatu safu ya uongozi mpya ni kama ifuatayo;
1.  Mwenyekiti - John F Kitime
2.  Makamu Mwenyekiti - Rashid Pembe
3.  Katibu Mkuu - Innocent Nganyagwa
4.  Katibu Mkuu Msaidizi - Geophrey Kumburu
5.  Mweka Hazina - Asha Warsama
6.  Wajumbe - David Ng'asi, Abdul Salvador
TAMUNET ni chama ambacho malengo yake ni kutetea haki za wanachama wake kama wafanyakazi katika tasnia, na kuwa chama rasmi cha wafanyakazi waliomo katika tasnia ya muziki (Musicians Union). Uongozi uliopo unajipanga kuhakikisha chama kinafanya kazi yake ambayo imo katika katiba yake. 
Picha za uongozi mpya wakiwa katika kikao




Friday, April 7, 2017

MWANAMUZIKI UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA FETE DE LA MUSIQUE?


Haya tena wanamuziki wenzangu tamasha la Fête de la Musique linawakaribisha wanamuziki wa kila aina kuomba kushiriki katika msimu wa sita wa tamasha litakalofanyika tarehe 17 mwezi juni 2017 Johannesburg, South Africa. Mwisho wa kupelka maombi ni Ijumaa tarehe 28 April 2017.

Namna ya kuomba

Wasanii wanaotaka kushiriki wapeleke maombi yao yakiambatana na :

·       Maelezo ya historia ya msanii (Artist biography)

·       Picha (Photo)

  • Maelezo ya kiufundi ya vifaa utavyotumia jukwaani (Technical rider)
  • Nakala ya muziki wako (Sound clips)
  • Videos
  • Maelezo yako yatakayoweza kutumika katika matangazo (Press kit)

Maombi yote yanaweza kutumwa kupitia fetedelamusiquejoburg@gmail.com wakati fomu za maombi zinapatikana  HAPA

Fête de la Musique ni tamasha ambalo linaweza kuhudhuriwa na familia nzima bila kujali rika, nia yake ikiwa ni kufurahia muziki wa’live’. Pia ni mahala ambapo wasanii kutoka nchi mbalimbali wanaweza kukutana.

Kwa kuwa kuna maelfu ya wapenzi wa muziki hukutana hapa katika tukio hilo la mara moja kwa mwaka, wanamuziki maarufu na wasio maarufu hupanda jukwaa moja. Tamasha lipo kwa hisani ya Alliance Francaise Johannesburg na French Institute of South Africa, wakishirikiana na Bassline Live kwa ufadhili wa Total.

Mwaka  2016, Fête de la Musique iliwakusanya karibu watu 8 000 katika mji wa Newtown, Johannesburg. Baadhi ya wasanii walioshiriki walikuwa Vaudou Game (France), Blk Jks (South Africa), Les Fantastiques (DRC), Jess & Crabbe (France), Bombshelter Beast (South Africa), Mapumba Cilombo (DRC), Morayks (Lesotho), Zanmari Baré (Reunion Island) na wengine wengi.

Wednesday, March 29, 2017

UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA SANAA UGANDA?


JE,  unataka kushiriki katika tamasha la Bayimba International Festival, ambalo litafanyika tarehe 15-17 September 2017  Kampala, Uganda?

Tamasha la mwaka huu litakuwa ni la kumi. Ni tamasha ambalo linajumuisha muziki, dansa, maonyesho jukwaani, filamu, vichekesho, mashahiri, na sanaa za maonyesho. Wanaohitaji kushiriki ni muhimu kuwa wameshajaza fomu zao na kutuma ifikapo April 30. Katika tamasha la mwaka jana walikuweko wasanii wa Hiphop kama  Akua Naru kutoka Ghana, Tribute ‘Birdie’ Mboweni toka Afrika ya kusini, bibie wa Kiganda ambae ni mpiga saxaphone wa mahadhi ya soul Mo Roots, kundi la Reggae toka Kenya Gravittii Band, na wengine wengi. Kutakuwepo na malipo kidogo kwa washiriki toka nje ya Uganda, japo washiriki wanashauriwa kutafuta njia za kulipia gharama za usafiri, viza na bima mbalimbali. Barua ya utambulisho itatolewa mara utakapokubaliwa kushiriki ili ikusaidie kutafuta ufadhili. Wanaotaka kushiriki wanatakiwa watoe taarifa zifuatazo,

·     Fomu ya ushiriki na kupitia bayimbafestival.com

·     Maelezo mafupi ya wasanii yasiyozidi maneno 800 na picha ya karibuni 

·     Nakala ya kazi yako, kama ni muziki au filamu kazi moja au mbili kwenye CD, DVD or mp3.

·     Mahitaji yako ya vifaa (technical rider/data sheet)

Watayarishaji watawajibu mapema waliofanikiwa.Fomu za maombi zinapatikana pia  HAPA