Thursday, October 26, 2017
Monday, October 16, 2017
UHURU FM WALIPOLIAMSHA DUDE JANA KWENYE VIWANJA VYA MWEMBEYANGA, TEMEKE, KATIKA TAMASHA LA 'GUSA MAISHA YAKE' KUMUENZI BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU NYERERE
Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere |
Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere |
Tamasha la Muziki Mnene laacha historia Jijini Mwanza
Binagi Media Group
Maelfu ya wapenzi
wa burudani Jijini Mwanza jana wamefurahia tamasha la Mziki Mnene
linaloandaliwa na EFM radio na ETV za Jijini Dar es salaa ambapo wasanii
mbalimbali akiwemo Kala Jeremiah walipata shangwe kubwa kwenye tamasha hilo
lililofanyika uwanja wa CCM Krumba.
Wasanii
wengine waliokonga nyoyo za mashabiki zao ni TID, Snura, Young Killer, Baraka
Da Prince, Shoro Mwamba pamoja na Msaga Sumu huku Stone Fire akiibuka mkali wa
Singeli Michano Mwanza baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 20.
Afisa Uhusiano
wa EFM Radio, Jesca Mwanyika anasema tamasha hilo mbali ya kuwa ni sehemu ya
shukurani kwa wasikilizaji wa redio hiyo pamoja na watazamaji wa TVE, pia
limelenga kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii hususani wa Singeli.
Tayari
limekwisha fanyika katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Mtwara na
Mwanza na kwamba litaendelea katika mikoa mingine hivyo mashabiki wa burudani
waendelee kufuatilia EFM Radio na TVE kwa taarifa mbalimbali ikiwemo tamasha la
Mziki Mnene linalopewa nguvu na Biko pamoja na Cocacola.
Mkali wa Singeli, Msaga Sumu akidondosha burudani kwenye jukwaa la Mziki Mnene CCM Kirumba Jijini Mwanza.Sunday, October 15, 2017
Saturday, October 14, 2017
TANZANIA WOMEN'S BANK YASHIRIKI KIKAMILIFU SIKU YA VICOBA TANZANIA
Banda la TWB au Tanzania Women's Bank lilikuwa moja ya mabanda ambayo yalikuwa mstari wa mbele kuhusu kutoa elimu stahiki kwa watumiaji wa benki hiyo katika siku hii ya Vicoba Tanzania. Vijana wachangamfu waliokuweko katika banda hili walikuwa tayari kutoa elimu yoyote ambayo mtu alitaka kupata kuhusu shughuli ya benki hii ya wote.
Sunday, July 16, 2017
RATIBA YA MSIBA WA MKE WA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO
Mke wa mheshimiwa Waziri wa habari Utamaduni na Michezo, Dr Harrison Mwakyembe, Bi Linah Mwakyembe amefariki usiku wa kuamkia jana Jumapili, katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam alikokuwa anatibiwa. Ratiba ya msiba ni kama ifuatavyo:
Jumanne 18/7/2017 asubuhi mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwa Mhe. Dr Mwakyembe Kunduchi Beach, kisha taratibu za Ibada na kuaga zitafuata na hatimae mwili kusafirishwa kwenda Kyela zitafanyika siku hiyohiyo. Mazishi yatakuwa Kyela siku ya Jumatano
Mungu Amlaze Pema Linnah Mwakyembe
Jumanne 18/7/2017 asubuhi mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwa Mhe. Dr Mwakyembe Kunduchi Beach, kisha taratibu za Ibada na kuaga zitafuata na hatimae mwili kusafirishwa kwenda Kyela zitafanyika siku hiyohiyo. Mazishi yatakuwa Kyela siku ya Jumatano
Mungu Amlaze Pema Linnah Mwakyembe
Wednesday, June 21, 2017
MTANDAO WA MUZIKI TAMUNET WAJIPANGA UPYA
Katika kuadhimisha Siku ya Muziki Duniani ambayo husherehekewa kila tarehe 21 June, wajumbe wa Mtandao wa Muziki, Tanzania Musicians Network, leo wamesherehekea kwa kufanya kikao kilichojenga kamati ya uongozi ya mud, viongozi hawa watakuwa katika uongozi kwa mwaka mmoja kisha kutayarisha Mkutano Mkuu wa kuchagua viongozi wa kudumu. Katika kikao cha leo kilichotumia masaa matatu safu ya uongozi mpya ni kama ifuatayo;
1. Mwenyekiti - John F Kitime
2. Makamu Mwenyekiti - Rashid Pembe
3. Katibu Mkuu - Innocent Nganyagwa
4. Katibu Mkuu Msaidizi - Geophrey Kumburu
5. Mweka Hazina - Asha Warsama
6. Wajumbe - David Ng'asi, Abdul Salvador
TAMUNET ni chama ambacho malengo yake ni kutetea haki za wanachama wake kama wafanyakazi katika tasnia, na kuwa chama rasmi cha wafanyakazi waliomo katika tasnia ya muziki (Musicians Union). Uongozi uliopo unajipanga kuhakikisha chama kinafanya kazi yake ambayo imo katika katiba yake.
1. Mwenyekiti - John F Kitime
2. Makamu Mwenyekiti - Rashid Pembe
3. Katibu Mkuu - Innocent Nganyagwa
4. Katibu Mkuu Msaidizi - Geophrey Kumburu
5. Mweka Hazina - Asha Warsama
6. Wajumbe - David Ng'asi, Abdul Salvador
TAMUNET ni chama ambacho malengo yake ni kutetea haki za wanachama wake kama wafanyakazi katika tasnia, na kuwa chama rasmi cha wafanyakazi waliomo katika tasnia ya muziki (Musicians Union). Uongozi uliopo unajipanga kuhakikisha chama kinafanya kazi yake ambayo imo katika katiba yake.
Picha za uongozi mpya wakiwa katika kikao
Wednesday, June 14, 2017
Friday, April 7, 2017
MWANAMUZIKI UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA FETE DE LA MUSIQUE?
Haya
tena wanamuziki wenzangu tamasha la Fête de la Musique
linawakaribisha wanamuziki wa kila aina kuomba kushiriki katika msimu wa sita
wa tamasha litakalofanyika tarehe 17 mwezi juni 2017 Johannesburg, South
Africa. Mwisho wa kupelka maombi ni Ijumaa tarehe 28 April 2017.
Namna ya kuomba
Wasanii wanaotaka kushiriki wapeleke
maombi yao yakiambatana na :
·
Maelezo ya historia ya msanii (Artist biography)
·
Picha
(Photo)
- Maelezo ya kiufundi ya vifaa utavyotumia jukwaani (Technical rider)
- Nakala ya muziki wako (Sound clips)
- Videos
- Maelezo yako yatakayoweza kutumika katika matangazo (Press kit)
Maombi
yote yanaweza kutumwa kupitia fetedelamusiquejoburg@gmail.com wakati
fomu za maombi zinapatikana HAPA
Fête
de la Musique ni tamasha ambalo linaweza kuhudhuriwa na familia nzima bila
kujali rika, nia yake ikiwa ni kufurahia muziki wa’live’. Pia ni mahala ambapo
wasanii kutoka nchi mbalimbali wanaweza kukutana.
Kwa
kuwa kuna maelfu ya wapenzi wa muziki hukutana hapa katika tukio hilo la mara
moja kwa mwaka, wanamuziki maarufu na wasio maarufu hupanda jukwaa moja.
Tamasha lipo kwa hisani ya Alliance Francaise Johannesburg na French Institute
of South Africa, wakishirikiana na Bassline Live kwa ufadhili wa Total.
Mwaka
2016, Fête de la Musique iliwakusanya
karibu watu 8 000 katika mji wa Newtown, Johannesburg. Baadhi ya wasanii
walioshiriki walikuwa Vaudou
Game (France), Blk Jks
(South Africa), Les Fantastiques (DRC), Jess & Crabbe (France), Bombshelter
Beast (South Africa), Mapumba Cilombo (DRC), Morayks (Lesotho), Zanmari Baré
(Reunion Island) na wengine wengi.
Subscribe to:
Posts (Atom)