KATIKA
hatua ya kujua mafanikio na changamoto za muziki wa dansi na hatimae
kupanga yajayo, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo atakutana na
wanamuziki wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Vijana Social Hall
Kinondoni siku ya Jumatatu kuanzia saa nne asubuhi. Hii itakuwa ni mara
ya kwanza kwa miaka mingi kwa Waziri wa Utamaduni kufanya mkutano wa
namna hii na wanamuziki.
Saturday, March 19, 2016
Sunday, February 21, 2016
LEO NDIO SIKU YA MAZISHI YA RAFIKI YETU NA NDUGU YETU FRED CAMILLIUS MOSHA
RIP FRED MOSHA |
RATIBA YA MAZISHI NI KAMA IFUATAYO;
- SAA 4-5 MWILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWAKE CHAMAZI UKITOKEA MUHIMBILI
- SAA 7 MWILI KUPELEKWA KANISA LA RC CHANG'OMBE KWA MISA YA MAZISHI
- BAADA YA HAPO SAFARI ITAANZA YA KUELEKEA MAKABURI YA KINONDONI KWENYE MAKAZI YAKE YA MILELE
- MUNGU MALAZE PEMA PEPONI FRED MOSHA
Tuesday, January 19, 2016
SIZONJE -KIBAO KIPYA CHA MRISHO MPOTO AKISHIRIKIANA NA BANANA ZOLLO
Mrisho Mpoto- mjomba amekuja na kibao kipya kabisa Sizonje, kibao ambacho kamshirikisha mwanamuziki Banana Zollo, kisikie hapa
Thursday, December 10, 2015
RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AUNDA WIZARA MPYA
Mhe Nape M Nnauye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo |
Rais John Pombe Magufuli ameunda Wizara mpya itakayoshughulikia pia wasanii. Katika kutangaza baraza jipya la mawaziri ambalo hakika litakuwa dogo kama alivyoahidi wakati wa kampeni, pia Ria amekuja na Wizara mpya. Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo. Waziri aliyeteuliwa ni Mheshimiwa Nape Moses Nnauye. Kwa wengine tuliomo katika Wizara hii hakika tunaona tunahitaji mabadiliko mengi, yakiwemo uongozi wenye uzalendo wa kupenda utamaduni wa Kitanzania, pia uongozi utakaotengeneza na kuheshimu mtiririko wa uongozi wa kiserikali wa shughuli za Utamaduni. Pia tungependa uongozi ambao unakubali kusikiliza pande zote za wadau wa tasnia ya sanaa. Uongozi ambao utaelewa tofauti kati ya Utamaduni, sanaa na burudani. Uongozi ambao utakuwa wa kwanza kuhakikisha sheria na taratibu zihusuzo sanaa zinafuatwa. Tuna uhakika Mheshimiwa Nape atayaweza haya na zaidi, hivyo kuweza kuweka kumbukumbu ya uwepo wake katika historia ya sanaa ya nchi hii. Bado jina la Wizara linaleta chemsha bongo katika kipengele cha wasanii, je Wizara itahusika na wasanii au Sanaa? Najua inawezekana likaonekana ni swali la ajabu lakini ukukikumbuka tu kuwa kuna wizara ya kilimo sio ya wakulima, au wizara ya biashara na si ya wafanyabiashara, kuna wizara ya uvuvi si ya wavuvi, ni mifano michache ya kuonyesha changamoto hii.
Monday, November 23, 2015
JOHN KITIME ATOA ELIMU YA HAKIMILIKI KWA VIONGOZI WA VYAMA NA VIKUNDI VYA SANAA
MWENYEKITI wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, John Kitime, siku ya tarehe 19 Novemba 2015, alitoa semina ya Hakimiliki kwa zaidi ya wasanii 50 waliokuwa katika warsha iliyoandaliwa na Baraza la Sanaa La Taifa (BASATA). Katika semina hiyo iliyotambulika kama Capacity Buildingfor Art Association and Group Leaders in Tanzania ilifanyika Ilala Shariff Shamba zilipo ofisi za BASATA. Kitime aliweza kuwafahamisha washiriki nini maana ya Hakimiliki, matumizi yake mipaka yake na kugusia sheria ya Hakimiliki ya Tanzania inavyofanya kazi. John Kitime ambaye amekwisha fanya semina za aina hii katika nchi mbalimbali Afrika zikiwemo Ghana, Malawi, Senegal amekwisha karibishwa Kenya kufanya semina za aina hiyo.
WASHIRIKI MBALIMBALI WAKIKABIDHIWA VYETU VYA USHIRIKI
STELLAH JOEL |
RAY |
BRAITON |
KAKA GANO |
Tuesday, November 17, 2015
TAMASHA LA KUMSHUKURU MUNGU SASA KUFANYIKA DESEMBA 25 DIAMOND JUBILEE
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akifafanua jambo kwa umakini mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani)
jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusu maandalizi ya tamasha la
kumshukuru Mungu kwa amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu litakalofanyika
Desemba 25.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusu maandalizi ya tamasha la
kumshukuru Mungu kwa amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu litakalofanyika
Desemba 25.
KAMPUNI ya Msama Promotions imeamua
kuandaa Tamasha la muziki wa Injili litakalofanyika katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumshukuru Mungu nchi kuvuka salama
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki,
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, alisema wameamua kuua ndege wawili kwa jiwe moja, kwani sasa litafanyika
Desemba 25, likibeba Sikukuu ya Krismasi na shukrani hiyo ya kuvuka salama
katika Uchaguzi Mkuu.
Alisema kutokana na tamasha hilo kubeba ajenda hizo mbili kwa pamoja, kamati
yake imelipa uzito mkubwa kwa upande wa suala la maandalizi ambapo wameanza kuzungumza na
waimbaji nguli wa kitaifa na kimataifa.
Msama alisema baada ya tamasha hilo
kufanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, litahamia katika mikoa
mbalimbali itakayoteuliwa na kamati yake kwa kuzingatia kigezo cha wingi wa
maombi na uwezo wao kifedha.
“Naomba ifahamike, tamasha hili la
kumshukuru Mungu kuiwezesha nchi kuvuka salama katika mtihani mgumu wa Uchaguzi
Mkuu uliokuwa na ushindani mkubwa, litafanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa
Diamond Jubilee,” alisema Msama na kuongeza:
“Unaweza kuona ni tamasha ambalo safari
hii litakuwa na uzito mkubwa, kwani litakuwa limebeba uzito wa Krismasi
itakayoambatana na shukrani maalumu kwa Mungu kutokana na kuijalia nchi kuvuka
salama katika Uchaguzi Mkuu,” alisisitiza Msama.
Kuhusu waimbaji, Msama alisema kamati
yake itajitahidi kuwaleta wenye uzito na mvuto kulingana na uzito wa tamasha hilo, akiamini litakuwa na
mvuto wa tofauti na yaliyotangulia na kuwasihi wapenzi na mashabiki wa muziki
wa Injili kukakaa mkao wa kupokea baraka za Mungu.
Msama kupitia Kampuni yake ya Msama
Promotions, amechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa Injili nchini
kupitia ubunifu wake wa kuratibu matukio ya muziki huo kuanzia tamasha la
Pasaka, Krismasi na uzinduzi wa kazi za waimbaji mbalimbali.
Juhudi hizo za Msama ndizo zimeufanya
muziki wa Injili kupata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kiasi cha kuwa
moja ya ajira kwa vijana wenye vipaji na karama ya kumtumikia Mungu kwa njia
hiyo ya uimbaji.
Thursday, November 12, 2015
KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO ATEMBELEA BASATA
Prof Elisante akiongea na akina mama wanaofanya sanaa ya kutengeneza Batik katika maeneo ya BASATA Toka kushoto Godfrey Mngereza, Katibu Mtendaji BASATA, Prof Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, John Kitime Mjumbe wa Bodi BASATA, Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni
KATIBU mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Vijana na Michezo Prof Elisante Ole Gabrielleo ametembelea Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Katibu MKuu baada ya kuzunguka na kuangalia maeneo yote ya Baraza, hatimae alikuwa na mkutano na wafanya kazi wa Baraza. Katika mkutano huo Katibu Mkuu alisema ametembelea Baraza ili kufahamiana,na pia kufafanua kauli mbiu ya Rais ya HAPA KAZI TU.
Katibu Mkuu alisifia Baraza kwa kusimamia sheria na taratibu zilizounda Baraza hilo. Profesa alilitaka Baraza kuhakikisha kuwa linakuwa na ufanisi zaidi na pia kuwezesha kutafuta masoko ya uhakika ya kazi za sanaa. Tanzania ina kazi nyingi sana za sanaa hivyo alilitaka Baraza kuhakikisha zinafahamika zinatangazwa, na zinasambazwa, ili kuleta manufaa kwa wasanii na kuchangia pato la nchi kwa kodi. Katibu Mkuu aliagiza kuwa viongozi wa Baraza wawe mfano katika utendaji wa kazi, heshima kwa watumishi wote na pia wawe waadilifu katika kazi zao. Katibu Mkuu aliwaasa watumishi wa Baraza kuipenda kazi yao kuwa wazalendo na kuwajibika ipasavyo, kuheshimu viongozi na kuwasiliana kwa staha pale kunapokuwa na tatizo. Aliwakumbusha wafanya kazi kuwahi kazini lakini pia alikumbusha uongozi kutokuwaweka wafanya kazi masaa ya ziada bila ya sababu za msingi, kwani wanahtaji kupumzika baada ya kazi za siku nzima. Aliwaonya watumishi kuhusu ‘majungu’ na kuwataka waepuka jambo hilo kwani ni chanzo cha kuharibu kazi. Kabla ya hotuba hii Katibu Mtendaji alimueleza Katibu Mkuu kuhusu changamoto za Baraza na baadhi ya njia ambazo zingefanywa kutatua changamoto hizo. Katibu Mkuu alisema kuwa yeye haridhiki na hali ya uchumi ya wasanii na alitaka Baraza lifanye kazi kubadili hali hii. Na mwisho alisisitika kuwa kauli ya Hapa Kazi tu ni ya ukweli na kila mtu aishi kwa kauli mbiu hiyo.
Kabla ya maelezo haya Katibu Mtendaji wa Basata alitoa baadhi ya changamoto za uendeshaji wa BASATA. Kati ya changamoto hizo alizitaja kuwa ni ukosefu wa sera za sanaa, kupitwa na wakati kwa sheria iliyounda Baraza. Mtawanyiko wa asasi zinazotawala wasanii. Ukosefu wa masoko ya sanaa, kutokukamilika kwa ukumbi wa BASATA, tatizo la siasa kujikita katika sanaa, na pia uhamasishaji wa Bima ya Afya kwa wasanii.
Katibu Mtendaji alimkabidhi Katibu Mkuu, nyaraka zote zilizotayarishwa kuhusu changamoto hizo
Thursday, October 29, 2015
KATIBU MTENDAJI WA BASATA AMKABIDHI MZEE MAPILI KADI YAKE YA BIMA YA AFYA
Katibu Mtendaji wa BASATA Bwana Ngereza, Mzee Mapili na Mama Shalua mmoja wa maafisa wa BASATA |
KUPITIA mpango unaoratibiwa na TAMUNET, ambapo Mtandao huu umeingia makubaliano na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa HHIF, mwanamuziki mkongwe wa siku ntingi ameweza leo kukabidhiwa kadi ya Bima ya Afya. Akikabidhiwa kadi hiyo Mzee Mapili alishukuru Mtandao wa Wanamuziki, na kusema kuwa mpango huu utamsaidia sana kwani ana matatizo ya moyo na figo na anahitaji matibabu na dawa za mara kwa mara. Katibu Mtendaji wa BASATA aliwashauri wanamuziki na wasanii wengine kujiunga na Bima ya Afya
Tuesday, October 27, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)