Sunday, September 15, 2013

MTANDAO WA MUZIKI TANZANIA WAPATA UFADHILI WA BEST AC


MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA umepata ufadhili kutoka Business Environment Strengthening of Tanzania (BEST – AC) ili kuweza kufanya utafiti wa kina kupata ukweli wa hali halisi ya ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha ya muziki unaofanywa na COSOTA, na baada ya hapo kutoa ushauri wa nini kifanyike ili kuboresha hali iliyopo. Madhumuni ya mradi huu ni kuwezesha kufanya mabadiliko katika tasnia ya muziki ambayo yatatengeneza nafasi za ajira zenye tija ili kuwezesha tasnia kutoa mchango wake katika pato la Taifa, na kukuza sifa ya nchi kutokana na wasanii wengi wenye sifa waliomo hapa nchini.

Mradi utaangalia sheria zilizopo zinazohusu ugawaji wa mirabaha ya wanamuziki na mambo mengine yote yanayohusiana na shughuli ya ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha na kupendekeza taratibu za kuboresha hali.

Kamati za fedha na utawala zitaanza kazi wiki hii ili kuweza kufanikisha zoezi hili ambalo linatakiwa likamilike katika muda wa mwezi mmoja. Wanamuziki watashirikishwa katika semina ambayo itafanyika katika wiki chache zijazo.  Mtafiti kutoka Afrika ya Kusini amekwisha ingia mkataba na Mtandao ili kufanya kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment