Thursday, August 22, 2013
Mwenyekiti na Mweka Hazina katika mafunzo ya siku tatu
Mwenyekiti wa Mtandao John Kitime na Mweka hazina wa Mtandao Bi Asha Salvador, wamo katika mafunzo ya siku tatu ya Public Policy Advocacy, mafunzo yanayoendelea UDSM
Friday, August 16, 2013
KICHEKESHO..MWANAMUZIKI NA NJAA ZAKE
Mwanamuziki mmoja alikuwa na tabia ya kukuta mkewe kampikia chakula kila alipotoka kazini usiku. Siku moja mkewe akawa anaumwa hakupika hivyo jamaa aliporudi hakukuta chakula akalazimika kulala njaa. Katika usingizi akaota ankula ugali wa nguvu. Asubuhi alipoamka akakuta katafuna kona nzima ya godoro
Wednesday, August 14, 2013
Sikiliza SIUMWI SIKU YA MSHAHARA ya Soggy The Hunter
Ndugu zangu baada ya kuufanyia mixing upya sasa naachia rasmi ngoma
yangu mpya SIUMWI SIKU YA MSHAHARA nikiwa na WATENGWA na imetengenezwa
ARUSHA chini ya DAZ NALEDGE naombeni msaada wenu.Ni aina ya Hip-hop
ngumu ambayo sijawahi kufanya miaka yangu yote miaka 18 kwenye muziki
Wanamuziki wakutana na kusafisha ofisi yao mpya.
Katika kuonyesha kuwa wako katika nia ya ujio mpya wanamuziki kadhaa walikutanika na kufanya usafi wa ofisi yao asubuhi ya leo. Samani za ofisi zinategemewa kuingizwa siku ya Alhamisi na baada ya hapo Katibu Mkuu Abraham Kapinga mwanamuziki mpiga gitaa wa Tanzanite Band atatoa ratiba ya matumizi ya ofisi.
Tuesday, August 13, 2013
MKUTANO WA WANAMUZIKI WAFANA
Ule mkutano ulioitishwa na Tanzania Musicians network (TMN) au Mtandao wa Wanamuziki Tanzania umekuwa wa mafanikio makubwa. Kwanza kwa mahudhurio ya wasanii mbalimbali wakiwemo wanamuziki wa muziki asili, taarab, dansi, bongoflava na gospel, pia kulikuweko na mameneja wa wanamuziki na mabendi mbalimbali, producers. Hii ilikuwa ni mafanikio makubwa kwani ilionyesha maana halisi ya mtandao.
Pamoja na maelezo ya madhumuni ya kutengeneza mtandao, mwenyekiti wa
Mtandao John Kitime alieleza kuwa wanamuziki wa Tanzania lazima
wafanye kazi ya ziada ili kuwakamata kimaendeleo wenzao wa nchi nyingine Afrika. Wanamuziki
walielezwa umuhimu wa kutumia teknolojia ya internet kwa kuhakikisha kuwa kila
mwanamuziki ana anwani ya barua pepe na kujitahidi kuingia kwenye mitandao ya
kijamii kama Facebook na kuitumia vizuri kwa kutangaza kazi zao. Wanamuziki
walikaribishwa kutumia blog yao ya www.tanzaniamusicians.blogspot.com
kwa kupeleka matangazo, picha za matukio mbalimbali hata ya shughuli binafsi
kama birthday, harusi na kadhalika
na pia kutuma hata nyimbo zao ili ziweze kutundikwa katika mtandao huo bure bila malipo.
Wanamuziki walielekezwa kutuma kazi zao kupitia anwani ya musicnettz@gmail.com.
Katibu Mkuu wa mtandao Abraham Kapinga, alitoa maelezo kuhusu
hali ya ofisi, ambapo wanamuziki walielezwa kuwa ofisi iko Kinondoni karibu na American
Chips, mtaa wa CHADEMA, na kwa vile ndio tumekabidhiwa ofisi, wanamuziki
waliafikiana kukutana hapo na kuifanyia ofisi usafi, jambo ambalo nalo lilionyesha nia ya wanamuziki kulea chama chao. Mwanamuziki Hussein Jumbe
alijitolea viti 4 kwa ajili ya ofisi, jambo ambalo kwa kila hali ni la kutia
moyo kuhusu mwanzo huu wa mtandao.
Mweka hazina wa Mtandao Asha Salvador alitoa taarifa ya
vifaa vya ofisi vilivyonunuliwa vikiwemo viti, meza feni, na stationary.
Maelezo mengine muhimu yaliyotolewa ni kuhusu wanamuziki
kujiunga na chama, na kulipia ada ili kuweza kuendesha ofisi. Fomu za wanachama
ni shilingi 1000/- ada ya mwaka 5,000/- na kiingilio ni shilingi 20,000/-.
Wajumbe walipata muda wa kutoa mawazo na mapendekezo. Mjumbe
mmoja alitoa mapendekezo ya mtandao kuwezesha wanamuziki kutoa maoni yao kuhusu
Rasimu ya Katiba ya nchi na mjumbe mmoja alijitolea kufuatilia
taratibu za kuhakikisha wanamuziki wanashiriki katika jambo hilo muhimu. Mjumbe mwingine alitaka Mtandao uandae
program za elimu ya Management ya Band na hata elimu kwa wanamuziki kujitambua
na hivyo sio kufika mahala kuporomoka baada ya muda mfupi, pia itolewe elimu
kuhusu haki mbalimbali za wanamuziki. Mmoja wa wajumbe alieleza kuwa ametoka
nje ya nchi karibuni alikopata elimu ya vocal training, na hivyo Mtandao uandae
taratibu ili elimu hii iwafikie wanamuziki waimbaji.
Mjumbe mmoja alitoa taadhari kuhusu hali inayoelekea sasa
ambayo inafanya kuweko na uhasama kati ya wanamuziki wa kizazi kipya na wale wa
zamani, badala ya wote kutambuana kuwa ni wanamuziki wanaoweza kufanya kazi
pamoja na kupata mafanikio makubwa zaidi, Mtandao uliombwa uwe chombo cha
kuunganisha wanamuziki wote bila kujali aina ya muziki wa rika.
Swala la vyombo vya utangazaji liliongelewa hasa kuhusu rushwa
iliyokithiri katika vyombo hivi ikawekwa hadharani. Mjumbe mmoja alieleza kuwa
imefikia kuwa inahitajika shilingi milioni moja kuwezesha wimbo kupigwa katika
radio, kwani kuna mgao wa kuanzia mtu anaweka nyimbo kwenye playlist hadi watangazaji wa vipindi mbalimbali kwa ajili ya kupiga muziki na interviews. Ilionekana tatizo hilo lipo hata kwenye radio zinazopiga muziki wa Gospel
ambako tofauti ni bei tu. Ambapo bei ya kupigwa wimbo ni kati ya shilingi alfu 80 hadi laki
moja. Mtandao ulitakiwa ufuatilie utekelezaji wa sheria ya kulipia matumizi ya
muziki katika vyombo vya utangazaji, ambayo ilikuwa ianze kutumika toka 2003.
Wanamuziki walimaliza siku kwa kutumia muda kujaza fomu za uanachama.
Sunday, August 11, 2013
MKUTANO WA WANAMUZIKI JUMANNE 13 AGOSTI 2013 BASATA
MTANDAO wa Wanamuziki utakuwa na mkutano wa wanamuziki siku ya Jumanne
tarehe 13 kuanzia saa 4 hadi saa 6 pale BASATA Ilala Sharif Shamba.kati ya mambo yatakayofanyika ni kuhamasisha uandikishaji wa wanachama wapya, na pili kupata taarifa ya mpango wa Bima ya Afya kwa wanamuziki. Wanamuziki wote na wadau wengine wanaofanya kazi katika tasnia hii ya muziki, wakiwemo pia waalimu wa muziki, producers, wacheza shoo, mameneja na kadhalika
Monday, August 5, 2013
UJUE MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA, hali halisi sasa na malengo kwa muda mfupi ujao
TANZANIA MUSICIANS NETWORK ni mkusanyiko ya wadau wote wanaofanya kazi kwa njia moja au nyingine katika tasnia ya muziki. Muziki hapa ukiwa na maana ya mapana yake yote, muziki wa vikundi na ule wa watu mmoja mmoja, na bila kuwa na mipaka ya aina ya muziki na bila kujali kama ni muziki asili au muziki mapokeo, hivyo kila mtu anaefanya kazi ya muziki bila kujali umaarufu wake au aina ya muziki wake anakaribishwa. Chama pia kinakaribishwa watendaji wengine katika muziki kama vile mameneja , maproducer wa audio na video, mafundi mitambo wa studio na wale wa 'live', dancers maarufu kama stageshow, na wachezaji wa ngoma za asili.
Wanachama wa Mtandao ni watu binafsi na si vikundi.
Mtandao una lengo la kuwakusanya wadau katika tasnia hii kuwa na sauti moja ili kuweza kurekibisha taratibu za utendaji katika tasnia hii na kuwawezesha wahusika wote kupata stahili zao kama inavyotakiwa. Mtandao ni mwanachama hai wa International Federation of Musician na hivyo moja ya malengo ya Shirikisho hilo ni kuhakikisha kazi ya muziki inatambuliwa kama ajira nyingine na hivyo kutungiwa sheria za kazi na taratibu za kazi kama kazi nyingine, na hivyo mtandao nao kulenga kufikisha hali hiyo kwa wanamuziki wa Tanzania. Kwa kipindi hiki cha awali ajenda nyingine kubwa ni kuweza kufanikisha kupatikana kwa Bima za Afya kwa wanamuziki wanachama mazungumzo yamekwisha anza na vyombo husika ili hili liwe limeanza kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwaka.
Kwa wakati huu Mtandao uko chini ya uongozi wa muda
Mwenyekiti: John Kitime -Mwanamuziki Kilimanjaro Band
Katibu Mkuu: Abraham kapinga- Mwanamuziki Tanzanite band
Mweka Hazina: Asha Salvador- mwanamuziki Hisia Sound
Mpaka sasa kuna kamati mbili, zenye wanamuziki mchakanyiko vijana na wakongwe, ambazo ziko kazini
i. kamati ya utawala ambayo imewezesha kupatikana kwa ofisi na baadhi ya vifaa vyake na sasa inaanza taratibu za uandikishaji wa wanachama
ii. kamati ya fedha ambayo inaratibu mapato na matumizi ya fedha.
Kamati ya tatu itaanza kazi kabla ya tarehe 15 mwezi huu ambayo itashughulikia na utayarishaji wa ripoti ya hali halisi ya shughuli za Hakimiliki, jambo ambalo litahusisha researchers wa ndani na nje ya nchi, workshop kubwa ya wanamuziki mwezi wa tisa, na hatimae shughuli nzima kutoa ripoti ambayo itaweza kutumika na vyombo mbalimbali vinavyohusika na muziki na ripoti itasaidia sana Serikali kuanza kutoa maamuzi sahihi.
Wanachama wa Mtandao ni watu binafsi na si vikundi.
Mtandao una lengo la kuwakusanya wadau katika tasnia hii kuwa na sauti moja ili kuweza kurekibisha taratibu za utendaji katika tasnia hii na kuwawezesha wahusika wote kupata stahili zao kama inavyotakiwa. Mtandao ni mwanachama hai wa International Federation of Musician na hivyo moja ya malengo ya Shirikisho hilo ni kuhakikisha kazi ya muziki inatambuliwa kama ajira nyingine na hivyo kutungiwa sheria za kazi na taratibu za kazi kama kazi nyingine, na hivyo mtandao nao kulenga kufikisha hali hiyo kwa wanamuziki wa Tanzania. Kwa kipindi hiki cha awali ajenda nyingine kubwa ni kuweza kufanikisha kupatikana kwa Bima za Afya kwa wanamuziki wanachama mazungumzo yamekwisha anza na vyombo husika ili hili liwe limeanza kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwaka.
Kwa wakati huu Mtandao uko chini ya uongozi wa muda
Mwenyekiti: John Kitime -Mwanamuziki Kilimanjaro Band
Katibu Mkuu: Abraham kapinga- Mwanamuziki Tanzanite band
Mweka Hazina: Asha Salvador- mwanamuziki Hisia Sound
Mpaka sasa kuna kamati mbili, zenye wanamuziki mchakanyiko vijana na wakongwe, ambazo ziko kazini
i. kamati ya utawala ambayo imewezesha kupatikana kwa ofisi na baadhi ya vifaa vyake na sasa inaanza taratibu za uandikishaji wa wanachama
ii. kamati ya fedha ambayo inaratibu mapato na matumizi ya fedha.
Kamati ya tatu itaanza kazi kabla ya tarehe 15 mwezi huu ambayo itashughulikia na utayarishaji wa ripoti ya hali halisi ya shughuli za Hakimiliki, jambo ambalo litahusisha researchers wa ndani na nje ya nchi, workshop kubwa ya wanamuziki mwezi wa tisa, na hatimae shughuli nzima kutoa ripoti ambayo itaweza kutumika na vyombo mbalimbali vinavyohusika na muziki na ripoti itasaidia sana Serikali kuanza kutoa maamuzi sahihi.
Sunday, August 4, 2013
MASHUJAA BAND YATAMBULISHA NYIMBO ZAKE ITAKAZO REKODI
Jana Jumamosi
tarehe 3 Agosti, bendi ya Mashujaa ilifanya jambo ambalo ni nadra
kufanyika katika bendi siku hizi. Bendi hii ilialika wadau na wapenzi wa bendi
ili waweze kuzisikiliza nyimbo ambazo bendi hii inatarajia kuzirekodi. Bendi
ilipiga mfululizo wa nyimbo tano,
zilizokuwa katika miondoko mbalimbali . Kwa ujumla bendi ina waimbaji wazuri
sana kadri ya mazingira ya uimbaji wa siku hizi. Nyimbo zilikuwa nzuri japo
zingeweza kuwa bora zaidi kwa kuongeza effects katika magitaa, na urekibishaji
wa sauti kwa ujumla(maarufu kama
setting) , japo ungeboreshwa zaidi. Tatizo la setting ya vyombo kwa ujumla
limekuwa sugu kwa bendi nyingi, kiasi kuwa kama ni kawaida kukuta sauti
zikitoka kwa kikwaruzo na mara nyingine kutosikia waimbaji wanatamka nini
katika wimbo.
Album hii itakuwa na mvuto kwa wapenzi wa muziki wa sebene,
na pia ni album ya kwanza baada ya bendi hii kubeba tuzo tano katika Kili Music
Awards karibuni.
Kati ya wadau waliokuweko katika shughuli hii ni wakali kama deo mwanatanga, William kaijage, Mafumu Bilali, Khalid Chokoraa, Khamis Dacota, John Kitime na wengine wengi walitoa mawazo yao kila baada ya wimbo kwisha ni jambo zuri kama litaendelezwa na pia kama litachukuliwa kwa uzito unaostahili na wanamuziki kwa upande wao.Saturday, August 3, 2013
TAAARIFA YA MSIBA--AGE KAUZENI HATUNAE TENA
Mwanamuziki
wa zamani wa Biashara Jazz Band na JUWATA Jazz Band Agae Kauzeni hatunae
tena. Kwa maelezo ya Mwanamuziki Bonzo Kwembe, marehemu amekuwa anaugua
kwa kipindi cha mwezi mmoja.Agai amefariki leo Visiga Kibaha. Na
mipango ya mazishi inafanyika ili mazishi yawe kesho Kibaha Mnemera.
Mungu Amlaze pema peponi
Wednesday, July 31, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)