Jana Jumamosi
tarehe 3 Agosti, bendi ya Mashujaa ilifanya jambo ambalo ni nadra
kufanyika katika bendi siku hizi. Bendi hii ilialika wadau na wapenzi wa bendi
ili waweze kuzisikiliza nyimbo ambazo bendi hii inatarajia kuzirekodi. Bendi
ilipiga mfululizo wa nyimbo tano,
zilizokuwa katika miondoko mbalimbali . Kwa ujumla bendi ina waimbaji wazuri
sana kadri ya mazingira ya uimbaji wa siku hizi. Nyimbo zilikuwa nzuri japo
zingeweza kuwa bora zaidi kwa kuongeza effects katika magitaa, na urekibishaji
wa sauti kwa ujumla(maarufu kama
setting) , japo ungeboreshwa zaidi. Tatizo la setting ya vyombo kwa ujumla
limekuwa sugu kwa bendi nyingi, kiasi kuwa kama ni kawaida kukuta sauti
zikitoka kwa kikwaruzo na mara nyingine kutosikia waimbaji wanatamka nini
katika wimbo.
Album hii itakuwa na mvuto kwa wapenzi wa muziki wa sebene,
na pia ni album ya kwanza baada ya bendi hii kubeba tuzo tano katika Kili Music
Awards karibuni.
Kati ya wadau waliokuweko katika shughuli hii ni wakali kama deo mwanatanga, William kaijage, Mafumu Bilali, Khalid Chokoraa, Khamis Dacota, John Kitime na wengine wengi walitoa mawazo yao kila baada ya wimbo kwisha ni jambo zuri kama litaendelezwa na pia kama litachukuliwa kwa uzito unaostahili na wanamuziki kwa upande wao.
No comments:
Post a Comment