Baada ya kazi nzuri ya awali Double M Sound chini ya
Muumin Mwinyjuma imealikwa tena Msumbiji. Kwa maneno yake mwenyewe kiongozi huyu
wa kundi hilo alituma ujumbe huu, “Nipo
njiani na vijana wangu tunaenda Msumbiji, tumepata mualiko mwingine, safari hii tumealikwa na
serikali kupitia Manispaa ya Mkoa Wa PEMBA, baada ya kufurahishwa na kazi yetu
ya mwezi uliopita. Kuna sherehe ya Kitaifa ambayo hua inazunguka kila Mkoa na
mwezi huu inafanyika ktk Mkoa Wa Mpemba, kutakua na burudani za aina nyingi tofauti. Safari Hii tumetakiwa kuwa na
idadi ya watu 14 tofauti na safari ya kwanza tulikwenda 19.
Kwenye msafara wetu tupo watu 13 na mwenzetu mmoja fundi
mitambo na mpiga tumba Omar Zagalo alibaki kule na vyombo toka tulipoenda mara
ya kwanza. Tulio kwenye msafara huu ni mimi Muumin Mwinyjuma, Rashid Sumuni-solo,
Pascal Kinuka-bass, Issa Ramadhani-kinanda, H Waninga-drums, Amina Juma, Salehe
Kupaza na Dogo Rama waimbaji, madansa
ni Verosa,Regina, Salma, Titi na Star. Tunasafiri kwa njia ya bus tukishavuka Boda
saa 10 Jioni tutachukuliwa na gari lililoandaliwa na wenyeji wetu, ambayo
itatumia saa 1-30 kutufikisha mji wa Msimbwe na hapo tutapanda ndege maalum itakayotupeleka
Pemba. Tuombeeni Mungu tufanye vizuri zaidi kwani Show hii ni muhimu sana
kujitangaza na kuutangaza muziki wa Bendi za TZ."