Monday, January 27, 2014
Friday, December 13, 2013
GURUMO 53 - TAMASHA LA KUSTAAFU MUZIKI MUHIDIN MAALI GURUMO
Wanamuziki kadhaa wenye heshima
katika muziki wa dansi watakuweko katika Tamasha la Gurumo 53, ambalo ni
tamasha la kustaafu muziki mwanamuziki mkongwe Muhidin Maalim Gurumo. Kati ya
wanamuziki watakao panda jukwaani ni
Komandoo Hamza Kalala, Mzee Makassy, wanamuziki nyota waliowahi kutamba
na bendi ya DDC Mlimani Park , Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe,
Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachala, Tshimanga Kalala Assossa,
Shaaban Lendi na Ibrahim Mwinchande. Pia wapulizaji wakongwe Majengo na King
Maluu watakuweko na wote kwa pamoja wataporomosha show kubwa Jumamosi
hii ndani ya TCC Club Chang’ombe. Wakali hao jana Alhamisi walihitimisha mazoezi ya nyimbo tano
watakazopiga katika tamasha hilo. Mazoezi hayo makali yalifanyika Amana Club
ambako kwa wiki nzima wanamuziki watakaoshiriki tamasha hilo wamekuwa
wakikutana hapo na kupiga mazoezi ya kufa mtu. Baadhi ya nyimbo zilizofanyiwa
mazoezi ni pamoja na “Selina”
utunzi wake Gurumo kwa kushirikiana na marehemu Joseph Mulenga, “Barua kutoka
kwa Mama” uliotungwa na Cosmas Chidumule na “Gama” (Tshimanga Kalala Assossa). Tamasha
la Gurumo 53 ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha miaka 53 ya utumishi uliotukuka
katika muziki wa dansi kwa Muhidin Maalim Gurumo ambaye ametangaza rasmi
kustaafu muziki. Wasanii wengine wanaoshiriki mazoezi hayo ni Miraji Shakashia,
Hafsa Kazinja, Juma Katundu, Edo Sanga. Burudani zingine zitakazokuwepo siku
hiyo ni pamoja na bendi za Msondo Ngoma Music Band, Talent Band, na Twanga
Pepeta.
Wednesday, November 20, 2013
MWENYEKITI WA MTANDAO ATOA MADA YA UTAFITI WA MALIPO YA MIRABAHA
Katika Jukwaa la Sanaa ambalo huweko kila Jumatatu katika ukumbi wa BASATA , wiki hii Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki John Kitime alichambua utafiti uliokamilika karibuni uliofanywa na mtafiti Martin Cuff kwa niaba ya Mtandao kwa ufadhili wa BEST AC. Utafiti huo ambao umo kwenye kitabu chenye kurasa 84 unachambua hali halisi ya Hakimiliki Tanzania, na mapungufu yake na kisha kutoa mapendekezo ya kuboresha hali hiyo kwa manufaa ya wenye Hakimiliki na tasnia ya muziki kwa ujumla. Kitabu cha utafiti huo kitapatikana baada ya muda si mrefu.
Thursday, November 7, 2013
UBALOZI WA MAREKANI WAKABIDHI VITABU 800 KWA MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA
Ubalozi wa marekani nchini Tanzania, leo hii 7/11/2013
umemkabidhi vitabu vya Hakimiliki zaidi ya 800 Mwenyekiti wa Tanzania
Musicians Network, John F Kitime katika hafla iliyofanyika katika maktaba ya
Ubalozi huo uliopo jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho chenye lugha mbili
Kiswahili na Kiingereza kimetungwa na Alex Perullo ambaye ni Associate Professor wa Anthropology na African Studieskatika chuo cha
Bryant Marekani. Hiki ni kitabu cha pili cha aina hii kutungwa na Profesa huyu,
cha kwanza alikisambaza kupitia Ubalozi huu huu miaka kumi iliyopita. Kwa vile
kina lugha mbili kitabu hiki kina majina mawili kinaitwa Artistic Rights na
Haki za Kisanii. Ni kitabu cha kurasa 98 ambacho kimejaa maelezo mengi kuhusu
haki za wasanii, wasanii watakao kisoma watafaidika sana.
Mtandao wa Muziki Tanzania, utakisambaza
kitabu hiki katika taasisi mbalimbali muhimu na pia utawapa bure wanachama wake
nakala za kitabu hiki muhimu. Dibaji ya kitabu hiki imeandikwa na John Kitime.
Wednesday, October 30, 2013
WANAMUZIKI WA TANZANIA WAFANYA WARSHA KUBWA
Martin Cuff |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya habari Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel ndie aliyefunga warsha hii kwa kusifu jitihada hii ya wanamuziki kufanya utafiti. Katika kukutana huku na Naibu Katibu mkuu wanamuziki walioingia mkataba na kampuni mojawapoya ringtones walilalamika kuwa waliingia mkataba wa miaka kumi na kampuni hiyo na baada ya hapo kampuni hiyo haikutaka hata kujibu barua zao, Naibu Katibu Mkuu aliwaita wahsanii hao ofisini kwake ili kuona cha kufanya, pia alimtaka Mwenyekiti wa Tanzania Musicians Network John Kitime amuone ili waongelee tatizo la TBC kutokulipa mirabaha na kuatafuta suluhu.
Monday, October 28, 2013
MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA WAFANYA WARSHA YA SIKU MOJA
WANAMUZIKI takriban 70 leo wameshinda siku nzima wakijadili ripoti ya utekelezaji wa Hakimiliki katika kipengele cha kukusanya na kugawa mirabaha. Wanamuziki wakiongozwa na mtafiti kutoka Afrika ya Kusin martin Cuff leo walifanya warsha hiyo katika ukumbi wa Nyumbani Lounge. Warsha ilifungwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya habari, Utamaduni na Michezo aliyesifu jitihada za wanamuziki kuweza kufanya kikao kama hiki.
Sunday, October 20, 2013
PRODUCERS WAHUDHURIA SEMINA YA HAKIMILIKI
Pamoja na kuwa leo ni siku ya Jumapili, watu wengi huwa wanapumzika, maproducer kadhaa wamejikusanya na kuhudhuria semina ya Hakimiliki iliyoendeshwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki John Kitime. Semina hiyo iliyofanyika katika jengo la Sayansi na Teknolojia iliwawezesha Producers kufahamu nini maana ya Hakimiliki na vilevile kupata elimu ya awali kuhusu yaliyomo katika sheria ya Hakimiliki ya hapa nchini
JULIUS NYAISANGAH.... UNCLE J.,,.SUPER TALL HATUNAE TENA
MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA UNATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA NDUGU , RAFIKI, NA WANAMUZIKI WALIOWAHI KUFANYA KAZI NA MTANGAZAJI MKONGWE JULIUS NYAISANGA, ALIYEFARIKI USIKU WA KUAMKIA LEO 20 OKTOBA, 2013 KATIKA HOSPITALI YA MAZIMBU MOROGORO.
MUNGU AMLAZE PEMA JULIUS, KAZI YAKO ULIOIFANYA KATIKA TASNIA YA MUZIKI HAITAFUTIKA
MUNGU AMLAZE PEMA JULIUS, KAZI YAKO ULIOIFANYA KATIKA TASNIA YA MUZIKI HAITAFUTIKA
Wednesday, October 16, 2013
Je unapenda muziki wa Mashujaa Band?
Bendi ya Mashujaa imetengeneza ukurasa wao ambapo unaweza sasa kusikiliza nyimbo zao nyingi kutoka hapo. Je wewe au bendi yako mnanyimbo katika mtandao wa intanet, basi tutumie anwani au wimbo kupitia musicnettz@gmail.com ili tuuweke katika blog yetu.
Kwa kusikiliza nyimbo za Mashujaa ingia HAPA upate nyimbo zao
Kwa kusikiliza nyimbo za Mashujaa ingia HAPA upate nyimbo zao
Thursday, October 3, 2013
KIPINDI CHA MIKIKI MIKIKI YA MUZIKI KUANZA KURUKA JUMAMOSI HII SAA 12:30 JIONI TBC RADIO YA TAIFA
BAADA ya kupata ufadhili wa BEST AC kwa kupitia Tanzania Heritage Project, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TMN), utaanza kurusha vipindi vya radio kupitia Radio TBC Taifa. Vipindi hivyo ambavyo vitaendeshwa na mwanamuziki na mwenyekiti wa Mtandao John Kitime. Kipindi cha kwanza kitaanza na kuangalia biashara ya muziki kwa kutegemea viingilio ilivyo na kama kweli inalipa na kitashirikisha kwa kukusanya maoni kutoka kwa wasikilizaji. Kipindi hiki ni mwanzo wa vipindi vingi vya redio vitakavyohusu muziki kama utamaduni, taaluma na kama biashara. Karibuni tusikilize na tutoe maoni kupitia blog hii na ukurasa wa facebook https://www.facebook.com/wanamuzikiwa.tanzania Wanamuziki wa Tanzania tuna uwezo kama wanamuziki wengine duniani lakini tuna matatizo makubwa ya mpangilio katika tasnia yetu
Subscribe to:
Posts (Atom)