BAADA ya kupata ufadhili wa BEST AC kwa kupitia Tanzania Heritage Project, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TMN), utaanza kurusha vipindi vya radio kupitia Radio TBC Taifa. Vipindi hivyo ambavyo vitaendeshwa na mwanamuziki na mwenyekiti wa Mtandao John Kitime. Kipindi cha kwanza kitaanza na kuangalia biashara ya muziki kwa kutegemea viingilio ilivyo na kama kweli inalipa na kitashirikisha kwa kukusanya maoni kutoka kwa wasikilizaji. Kipindi hiki ni mwanzo wa vipindi vingi vya redio vitakavyohusu muziki kama utamaduni, taaluma na kama biashara. Karibuni tusikilize na tutoe maoni kupitia blog hii na ukurasa wa facebook https://www.facebook.com/wanamuzikiwa.tanzania Wanamuziki wa Tanzania tuna uwezo kama wanamuziki wengine duniani lakini tuna matatizo makubwa ya mpangilio katika tasnia yetu
Yaani mngejua na mngeniona ninavyopumua haraka haraka kwa furaha na kiwewe, mngelinishangaa.
ReplyDeleteUKWELI NI KWAMBA KUANZA KWA KIPINDI HIKI NDIYO MWANZO WA KUURUDISHA MUZIKI WETU ULIOPOTEA.
SHIME WENZANGU TUTOE MICHANGO NA MAONI YETU