Tutakukumbuka daima Mzee Samwel John Sitta
Tuesday, November 8, 2016
PUMZIKA KWA AMANI SAMWEL JOHN SITTA
Mzee Samwel John Sitta alikuwa rafiki mkubwa wa wasanii na jambo ambalo wengi hawalijui ni kuwa pia alikuwa msanii mpiga gitaa. Mwalimu wa Mzee Sitta ambaye nae ni marehemu Mzee Brown Swebe aliwahi kusema kuwa alimfundisha gitaa Mzee Samweli Sitta wakati yuko shule ya sekondari Tabora, na alifanya hivyo kwa malipo ya kulima matuta kadhaa ya viazi. Wakati wote alikuwa kigusia umuhimu wa Hakimiliki na hata wakati akiwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba aliwezesha wasanii kukutana na wajumbe wengi wa Bunge la katiba kuweza kujielezea kuhusu umuhimu wa ulinzi wa mali isiyoshikika kutajwa katika katiba.
Tutakukumbuka daima Mzee Samwel John Sitta
Tutakukumbuka daima Mzee Samwel John Sitta
Friday, October 21, 2016
MZEE KUNGUBAYA AZIKWA NA WENGI
MWANAMUZIKI mkongwe ambaye alipata umaarufu kutokana na wimbo wake Salam za Wagonjwa amezikwa leo katika makaburi ya kifamilia Njeteni Kwembe. Msiba huo ulihudhuria na watu wengi wakiwemo majirani, ndugu, wanamuziki na wapenzi wa muziki wa Mzee Kungubaya.Tatu itakuwa siku ya Jumamosi 22/10/2016.
Jeneza likiwa nje ya nyumba ya marehemu |
Mwanamuziki Mjusi Shemboza akiongea na mmoja wa watoto wa marehemu Mzee Kungubaya |
Mjusi Shemboza akiwa na Mtendaji Mkuu wa COSOTA wa zamani Mzee Mtetewaunga |
Msafara wa kuelekea makaburini |
Mazishi ya Mzee Kungubaya |
Thursday, October 20, 2016
MZEE OMARI KUNGUBAYA HATUNAE TENA
Mzee Omari Kungubaya akipiga gitaa siku ya mkesha wa msiba wa Dr. Remmy Ongala |
Thursday, October 13, 2016
NGUZA VIKING, PAPII KOCHA NA TWANGA PEPETA JUKWAA LA TAMASHA LA WAFUNGWA
Bendi ya African Stars, maarufu kwa jina la Twanga Pepeta
kesho itashiriki katika Tamasha la Wafungwa ambalo litaanza saa 2 asubuhi.
Katika mambo ambayo yatakuwa makubwa kimuziki ni kushiriki kwa mwanamuziki
mkongwe Nguza Viking na mwanae
Papii Kocha ambao kwa sasa wanatumikia kifungo cha maish katika gereza la
Ukonga. Pia katika tamasha hilo atakuweko msanii nyita wa muziki wa Singeli
Msaga Sumu. Lengo la tamasha hilo ni kuwatia moyo wafungwa na kuwaonyesha kuwa
wapo pamoja na Watanzania wenzao walio nje ya magereza. Eric Shigongo
Mkurugenzi mkuu wa Global Publishersambao ndio walioandaa tamasha amesema hii
ni mara ya pili kuandaa tamasha la namna hii, ambalo lengo ni kunyanyua ari ya
wafungwa. Wafungwa waliohudhuria tamasha lililopita ambao walikwisha maliza
kifungo wamesifu na kusema tamasha lililopita liliwapa faraja sana. Mratibu wa
tamasha hilo Juma Mbizo, amesema mbali na burudani kali kutoka kwa Twanga,
kutakuwepo na michezo mbalimbali kama ya mpira wa miguu, kuvuta kamba na
mingineyo ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi. Pamoja na maneno mazuri ya kutia moyo
yatakayotolewa na Eric Shigongo, Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen
Mwaisabila naye anatarajiwa kutoa neno katika tamasha hilo sanjari na viongozi
wengine wa Jeshi la Magereza.
Saturday, October 8, 2016
RATIBA YA MSIBA WA MAREHEMU SALOME KIWAYA
Taarifa
ya ratiba ya msiba wa marehemu Salome Kiwaya aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma
na mwanamuziki, aliyefariki jana 07/10/2016, kwa ajali ya gari maeneo ya Kilimo Kwanza
Dodoma Mjini. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Image, Kata ya Kilimani,
Wilaya ya Dodoma Mjini. RATIBA:
1.Tarehe 08/10/2016 - maombolezo yanaendelea nyumbani Image Kilimani Dodoma.
2.Tarehe
09/10/2016 kuanzia saa 2:00 asubuhi - mwili wa marehemu utaletwa nyumbani
kutoka chumba cha maiti cha General
Hospital Dodoma.
3.
Tarehe 09/10/2016 saa kuanzia 6:00 mchana -salamu mbalimbali za Viongozi na Makundi
Maalumu zitaanza kutolewa.
Saa
8: 00 mchana- mwili wa marehemu utatolewa nyumbani, na kuelekea Kanisa Kuu Roman
Catholic. Baada ya Misa, msafara wa mwili wa marehemu utaelekea Kijiji cha Mtila,
Kata ya Matola Mkoa wa Njombe kwa ajili ya maziko tarehe 10/10/2016 siku ya
Jumatatu.
Friday, October 7, 2016
RIP SALOME KIWAYA
Picha iliyopigwa Uingereza wakati Salome alipoenda huko na Shikamoo Jazz Band. Toka Kushoto Marehemu Salome Kiwaya, Marehemu Papa Wemba, na Marehemu Bi Kidude Mungu awalaze pema. |
Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa za msiba wa Mama
Salome Kiwaya, mwanamuziki mkongwe. Taarifa zilinifikia kuwa Salome amefariki
katika ajali ya gari iliyotokea Dodoma sehemu za Meriwa. Nilimfahamu Salome kwa mara ya kwanza mwaka 1987, wakati nikiwa bendi ya Tancut Almasi Orchestra, tulipopiga kambi Dodoma Hotel
kwa muda wa miezi mitatu, tukitoa burudani kwanza kwa wajumbe wa mkutano wa Kizota, kisha wenyeji wa mji wa Dodoma. Katika kufahamiana kipindi hicho, tuliweza hata kupiga wimbo wake mmoja ulioitwa Tuhina, uliokuwa ukiimbwa na Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa, ambao nao ni marehemu. Siku moja nilipita mtaani Dodoma na
kununua kanda za muziki wa Salome, nilizipenda sana nyimbo zake na nikamuahidi kuwa ningejitahidi
kuzipeleka kwa watu wenye uwezo wa kuendeleza kazi zile. Nilizipeleka kanda kwa Ronnie
Graham, Mscotch mmoja mwenye upenzi na uelewa mkubwa wa muziki wa Kiafrika na
hasa rumba, na huyu Mscotch ndie aliyewezesha kuanzishwa kwa bendi ya Shikamoo Jazz Band.
Baada ya kuzisikia nyimbo zile akaamua kuwa Salome asindikizane na bendi ya
Shikamoo kwenye ziara yao ya Uingereza kama muimbaji wa kike. Salome alienda
Uingereza na aliporudi ndipo alipoanza kununa vyombo na kuunda kundi la Saki
Stars, ikiwa ni kifupi cha Salome Kiwaya Stars. Mume wake Mzee Kiwaya nae ni
msanii maarufu aliyekuwa kiongozi wa kikundi cha Utamaduni cha CDA miaka hiyo ya 80.
Kuanzia hapo nimekuwa karibu sana na Salome, miaka ya 90 wakati nikiwa
Mwenyekiti wa CHAMUDATA, Salome ndie alikuwa mwenyekiti wa chama hicho katika
mkoa wa Dodoma baada ya mkutano mkubwa wa wanamuziki uliofanyika mwezi June
1998, kule Bagamoyo, ambapo wanamuziki 265 waliweza kukusanyika pamoja na kukaa
siku nne katika mji wa Bagamoyo wakifanya warsha za fani mbalimbali za muziki.
Katika miaka ya karibuni Salome alishughulika na sanaa ya urembo akiwa wakala wa Miss Tanzania kwa kanda ya Kati na kuweza kutoa MIss Tanzania mmoja, baadae aliingia katika siasa na kufikia kuwa Mwenyekiti wa UWT wa Mkoa wa Dodoma, lakini aliendelea na muziki katika maisha yake
yote.
Mungu Amlaze Pema Salome Kwaya. Ucheshi wako hatutausahau.
JOHN KITIME
JOHN KITIME
Saturday, March 19, 2016
WAZIRI NAPE NNAUYE KUKUTANA NA WANAMUZIKI JUMATATU 21 MARCH 2016
KATIKA
hatua ya kujua mafanikio na changamoto za muziki wa dansi na hatimae
kupanga yajayo, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo atakutana na
wanamuziki wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Vijana Social Hall
Kinondoni siku ya Jumatatu kuanzia saa nne asubuhi. Hii itakuwa ni mara
ya kwanza kwa miaka mingi kwa Waziri wa Utamaduni kufanya mkutano wa
namna hii na wanamuziki.
Sunday, February 21, 2016
LEO NDIO SIKU YA MAZISHI YA RAFIKI YETU NA NDUGU YETU FRED CAMILLIUS MOSHA
RIP FRED MOSHA |
RATIBA YA MAZISHI NI KAMA IFUATAYO;
- SAA 4-5 MWILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWAKE CHAMAZI UKITOKEA MUHIMBILI
- SAA 7 MWILI KUPELEKWA KANISA LA RC CHANG'OMBE KWA MISA YA MAZISHI
- BAADA YA HAPO SAFARI ITAANZA YA KUELEKEA MAKABURI YA KINONDONI KWENYE MAKAZI YAKE YA MILELE
- MUNGU MALAZE PEMA PEPONI FRED MOSHA
Tuesday, January 19, 2016
SIZONJE -KIBAO KIPYA CHA MRISHO MPOTO AKISHIRIKIANA NA BANANA ZOLLO
Mrisho Mpoto- mjomba amekuja na kibao kipya kabisa Sizonje, kibao ambacho kamshirikisha mwanamuziki Banana Zollo, kisikie hapa
Subscribe to:
Posts (Atom)