Bendi ya African Stars, maarufu kwa jina la Twanga Pepeta
kesho itashiriki katika Tamasha la Wafungwa ambalo litaanza saa 2 asubuhi.
Katika mambo ambayo yatakuwa makubwa kimuziki ni kushiriki kwa mwanamuziki
mkongwe Nguza Viking na mwanae
Papii Kocha ambao kwa sasa wanatumikia kifungo cha maish katika gereza la
Ukonga. Pia katika tamasha hilo atakuweko msanii nyita wa muziki wa Singeli
Msaga Sumu. Lengo la tamasha hilo ni kuwatia moyo wafungwa na kuwaonyesha kuwa
wapo pamoja na Watanzania wenzao walio nje ya magereza. Eric Shigongo
Mkurugenzi mkuu wa Global Publishersambao ndio walioandaa tamasha amesema hii
ni mara ya pili kuandaa tamasha la namna hii, ambalo lengo ni kunyanyua ari ya
wafungwa. Wafungwa waliohudhuria tamasha lililopita ambao walikwisha maliza
kifungo wamesifu na kusema tamasha lililopita liliwapa faraja sana. Mratibu wa
tamasha hilo Juma Mbizo, amesema mbali na burudani kali kutoka kwa Twanga,
kutakuwepo na michezo mbalimbali kama ya mpira wa miguu, kuvuta kamba na
mingineyo ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi. Pamoja na maneno mazuri ya kutia moyo
yatakayotolewa na Eric Shigongo, Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen
Mwaisabila naye anatarajiwa kutoa neno katika tamasha hilo sanjari na viongozi
wengine wa Jeshi la Magereza.
No comments:
Post a Comment