Tuesday, October 27, 2015
Monday, October 26, 2015
DIAMOND ATWAA TUZO YA MTVEMA
HAKIKA Diamond kiboko yao. TAMUNET inatoa hongera kwa Diamond Platnumz kwa kushinda MTV
European Music Awards (MTVEMA), katika tukio lililofanyika Milan Jumapili hii tarehe 25 October wakati Tanzania ikipiga kura
kutafuta viongozi wake wa miaka mitano ijayo. Tuzo hili hufanyika katika miji mbalimbali ya Ulaya
kila mwaka, na washindi huchaguliwa kwa kura za wapenzi kutoka dunia nzima. Mcheza
filamu kutoka India na ambae pia alikuwa Miss World mwaka 2000 Priyanka Chopra pia alishiriki akiwa kundi
moja na Diamond, katika ‘ category ‘ ya
Worldwide Act : "Africa/ India". Pamoja na uwingi wa watu wa
India , Diamond Platnumz ameweza kupata kura nyingi zaidi na kuongeza sifa wake
mwenyewe binafsi na kwa Taifa. Hongera tena Diamond
Priyanka Chopra |
Saturday, October 24, 2015
Profesa Elisante Ole Gabriel ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne
wapya wa wizara mbali mbali. Kati Makatibu Wakuu hao Rais amemteua
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, kuwa Katibu Mkuu na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba
Nkinga kuhamishiwa Wizara ya Wanawake, Jinsia
na Watoto kutoka Wizara ya Habari. Hakika hii ni habari nzuri kwa wasanii katika kipindi hiki tunapongojea matokeo ya uchaguzi Mkuu. Profesa ni mchapa kazi wa ukweli, ni kati ya mambo mazuri makubwa yaliyotokea katika Wizara hii kwa muda mrefu
Wednesday, October 21, 2015
DOUBLE M WAKO MSUMBIJI KWA MARA YA PILI
Baada ya kazi nzuri ya awali Double M Sound chini ya
Muumin Mwinyjuma imealikwa tena Msumbiji. Kwa maneno yake mwenyewe kiongozi huyu
wa kundi hilo alituma ujumbe huu, “Nipo
njiani na vijana wangu tunaenda Msumbiji, tumepata mualiko mwingine, safari hii tumealikwa na
serikali kupitia Manispaa ya Mkoa Wa PEMBA, baada ya kufurahishwa na kazi yetu
ya mwezi uliopita. Kuna sherehe ya Kitaifa ambayo hua inazunguka kila Mkoa na
mwezi huu inafanyika ktk Mkoa Wa Mpemba, kutakua na burudani za aina nyingi tofauti. Safari Hii tumetakiwa kuwa na
idadi ya watu 14 tofauti na safari ya kwanza tulikwenda 19.
Kwenye msafara wetu tupo watu 13 na mwenzetu mmoja fundi
mitambo na mpiga tumba Omar Zagalo alibaki kule na vyombo toka tulipoenda mara
ya kwanza. Tulio kwenye msafara huu ni mimi Muumin Mwinyjuma, Rashid Sumuni-solo,
Pascal Kinuka-bass, Issa Ramadhani-kinanda, H Waninga-drums, Amina Juma, Salehe
Kupaza na Dogo Rama waimbaji, madansa
ni Verosa,Regina, Salma, Titi na Star. Tunasafiri kwa njia ya bus tukishavuka Boda
saa 10 Jioni tutachukuliwa na gari lililoandaliwa na wenyeji wetu, ambayo
itatumia saa 1-30 kutufikisha mji wa Msimbwe na hapo tutapanda ndege maalum itakayotupeleka
Pemba. Tuombeeni Mungu tufanye vizuri zaidi kwani Show hii ni muhimu sana
kujitangaza na kuutangaza muziki wa Bendi za TZ."
Tuesday, October 20, 2015
MSONDO NGOMA WAKUBALIANA KUPATA BIMA YA AFYA.
KATIKA mkutano uliofanyika leo kwenye makao makuu ya MSONDO, wanamuziki waliweza kupata taarifa ya namna BIMA YA AFYA inavyofanya kazi. Maelezo hayo yaliyotolewa kwao na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki, (TAMUNET) John Kitime. Baada ya mkutano huo wanamuziki hao walikubaliana kuanza kuhakikisha kila mmoja wao ana Bima ya Afya mara moja
Sunday, October 11, 2015
DIAMOND AZOA TUZO TATU AFRIMMA AWARDS
- Eddy Kenzo (Uganda)
- Jaguar (Kenya)
- Diamond Platnumz (Tanzania)
- Bebe Cool (Uganda)
- Jackie Gosse (Ethiopia)
- Ali Kiba (Tanzania)
- Dynamq (Sudan)
- Khadija Kopa (Tanzania)
- Aster Aweke (Ethiopia)
- Victoria Kimani (Kenya)
- Vanessa Mdee (Tanzania)
- Juliana Kanyamozi (Uganda)
- STL (Kenya)
- Irene Ntale (Uganda)
Best Newcomer
- Kiss Daniel (Nigeria)
- Pappy Kojo (Ghana)
- Korede Bello (Nigeria)
- Lil Kesh (Nigeria)
- Mz Vee (Ghana)
- Fabregas (Congo)
- Ommy Dimpoz (Tanzania)
- Bebi Philip (Ivory Coast)
- mpata Wapi’ (Tanzania)
- Sauti Sol – ‘Sura Yako’ (Kenya)
- Cassper Nyovest – ‘Doc Shabaleza’ (South Africa)
- Flavour (Nigeria)
- Diamond Platnumz (Tanzania)
- Sarkodie (Ghana)
- Cassper Nyovest (South Africa)
- Davido (Nigeria)
- Fally Ipupa (Congo)
- Eddy Kenzo (Uganda)
- Wizkid (Nigeria)
- Yemi Alade (Nigeria)
- Bucie (South Africa)
- Bracket ft. Diamond & Tiwa Savage – ‘Alive’ (Nigeria & Tanzania)
- Irene Ntale – ‘Woman’ (Uganda)
- Sarkodie ft. Castro – ‘Adonai’ (Ghana)
- Jose Chameleon – ‘Bwerere’ (Uganda)
- Psquare ft. Dave Scott – ‘Bring it On’ (Nigeria)
- Eddy Kenzo – ‘Be Happy’ (Uganda)
Thursday, October 8, 2015
TAMUNET YAFANYA MKUTANO
Wa kwanza kushoto, Abraham Kapinga (Tanzanite Band) Katibu Mkuu wa Mtandao |
Toka kushoto-Innocent Nganyagwa, Ally Jamwaka(Sikinde), Rashid Pembe(Mark Band), Davidi Ng'asi(Mwalimu wa muziki) |
Abdul Salvador |
Ilionekana kuwa kasi ya kujiunga na bima ya afya bado ni ndogo, na moja ya sababu ni ukosefu wa uelewa kuhusu umuhimu wa Bima na namna ya utendaji wa Bima. Mikakati ilipangwa kukabili hali hiyo.
Taaarifa ya Tamasha ilikwisha anza kusambazwa kutumia mitandao ya Facebook, vikundi vya Whatsapp Blog hii na taarifa za mdomo. Tayari wasanii kadhaa walionyesha nia ya kushiriki. Mtandao uangalie namna ya kwezesha wanamuziki hawa kufanikiwa katika ushiriki wa tamasha hili.
Ilikuablika kuwa katika wiki mbili zijazo kufanyike kikao cha kuangalia utekelezaji wa kushiriki katika kuboresha elimu ya muziki. Mwanamuziki na Mwalimu wa Muziki David Ng'asi alipewa jukumu la kuja na andiko la awali la mkakati huo.
Monday, October 5, 2015
Tuesday, September 29, 2015
MWANAMUZIKI WA DOUBLE M SOUND AVAMIWA NA VIBAKA MSUMBIJI
Taarifa
zimetufikia kwenye ofisi ya Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, kutoka kwa Muumin Mwinjuma 'Kocha' zikieleza kuwa mmoja wanamuziki wake
aliokuwa nao katika safari ya Msumbiji amepata mkasa wa kuibiwa na kuumizwa muda mfupi kabla ya onyesho kumalizika rasmi. Kwa kadri ya maelezo ya Muumini, bendi ilipiga katika
kitongoji cha Nanyupu, ambapo show hiyo ilikuwa ni ya pili katika mahala hapo
baada ya bendi kufanya show ya kwanza siku ya Jumapili tarehe 20 Septemba.
Kitongoji hiki ni makazi ya wachimbaji wa madini ya Ruby ambapo wengi wao ni
Watanzania, pia kuna wenyeji ambao ni Wamsumbiji, Wasenegali na Wanaijeria
kadhaa. Kwa kuwa Watanzania ni wengi, mara baada ya show ya kwanza, wakazi walimuomba aliyeipeleka bendi wakapige
show nyingine, nae hakukataa kwani alikuwa katengeneza pesa vizuri, hivyo bendi
ilikwenda kupiga tena siku ya Alhamisi tarehe 24 Septemba, siku ya Idd. Wakati
wa kupiga wimbo wa mwisho, muimbaji Amina hakuwa na kazi hivyo alishauriana na madansa watangulie kwenye gari. Madansa waliondoka kwa pamoja na kuelekea
kwenye gari lakini Amina ambaye pia ni katibu wa bendi alipanda kwanza jukwaani
kumuaga Muumini. Aliposhuka kwenye jukwaa kuelekea kwenye gari kundi la vijana
wakaanza kumsemesha Kiswahili nae akawa anajisikia kama yuko na ndugu zake.
Vijana wale ghafla wakamvamia na kuanza kumpiga makofi na kumburula na kumpora
mkoba wake uliokuwa na passport yake na ya mpiga drum na fedha za Msumbiji zenye thamani ya 150,000/-. Wenzie walipofika
kumsaidia tayari vibaka wale walikuwa wameshaingia gizani. Na mara moja dansi lilivunjwa ili
kumpeleka mji wa Pemba kwa matibabu.
Bendi
ilifanya maonyesho mengine mawili katika mji wa Pemba na kuona kuna haja ya kurudi kwanza nyumbani ili Amina apone vizuri, wakati wanamuziki wengine wanategemea kurudi nchini wakati wowote, Amina ataendelea kuwa Msumbiji kwa wiki moja zaidi ili apate matibabu zaidi. Pia bendi inakuja kujipanga kwa safari ndefu zaidi
inayotegemewa muda si mrefu.
Amina akiwa na mwanamuziki mwenzie Kupaza |
Monday, September 21, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)