Friday, August 29, 2014
MTANDAO WA MUZIKI WASHIRIKI SAFARI YA KUTEMBELEA BUNGE LA KATIBA DODOMA
Hii ndio PRESS RELEASE iliyosomwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa
Wanamuziki siku ya 27 August 2014 kwa waandishi wa habari jijini
Dodoma. Ndugu waandishi wa habari, katika mfumo wa sanaa wa nchi
yetu wasanii wamegawanyika katika makundi makuu manne, ambayo yanaendeshwa na
Mashirikisho ya vyama mbalimbali vya sanaa. Mashirikisho hayo ni;
i.
Shirikisho la Filamu TAFF
ii.
Shirikisho la Sanaa za Maonyesho
iii.
Shirikisho la Sanaa za Ufundi
iv.
Shirikisho la Muziki
Tuliopo mbele
yenu ni viongozi na wasanii kutoka vyama na Mashirikisho ya sanaa yaliyotajwa
hapo juu. Kundi hili limekuwepo hapa Dodoma kwa siku mbili kukutana na wajumbe
wa Bunge la katiba ili kufuatilia maslahi ya wasanii katika katika mchakato wa Katiba mpya ya nchi yetu Tanzania. Hii si mara ya kwanza kwa kundi hili
kukutana na Wabunge wa Bunge hili la Katiba, bali hii ni mara ya tatu kundi
hili limefika hapa Dodoma. Mchakato uliotufikisha leo hapa ulianza kwa
Mashirikisho kukutana na kutengeneza Baraza la katiba ambapo mashirikisho
yalitoa mapendekezo kadhaa yaliyofikishwa kwenye Tume ya Katiba. Lakini
hakukuweko jambo lolote lililotokana na mawazo hayo ambalo lilichukuliwa na
kuingizwa kwenye Rasimu ya Katiba. Mashirikisho yalituma majina 36, (tisa
kutoka kila shirikisho) katika
kupendekeza wawakilishi katika Bunge la Katiba. Katika hili mjumbe mmoja,
Paulynus Raymond Mtenda aliteuliwa na hivyo kubeba uwakilish wa kundi zima la
wasanii Tanzania. Siku ya Ijumaa 14/2/2014 Mashirikisho yote ya sanaa
yalikutana BASATA na kumkabidhi rasmi mapendekezo yao Mbunge huyu, ili
ahakikishe kundi hili haliachwi katika mchakato wa Katiba.
Muda mfupi baada ya hapo kundi hili lilikuja Dodoma, na
kukutana na Wabunge mbalimbali wa Bunge hili la Katiba, tulikutana na Wabunge
wa kambi zote na kufanya nao mikutano mingi, ambayo mingine ilifika mpaka saa
nane za usiku. Wabunge wa kambi zote walionekana kuunga mkono hoja za wasanii
na tulianza mawasiliano mbalimbali na Wabunge yakiwemo ya ana kwa ana, simu na
email, Wabunge wakihitaji documentation mbalimbali kuhusiana na mapendekezo
yetu katika Katiba mpya. Katika
kipindi hiki tulikuja wakati hata Mwenyekiti wa Bunde la Katiba hajachaguliwa.
Ujumbe huu ulikuja tena …. Na hii ni mara ya tatu.
Ujumbe huu toka awali ulikuwa na maombi mawili tu.
i.
Wasanii kutambuliwa kama kundi maalumu kama
yalivyotambuliwa makundi ya wakulima wafugaji, wavuvi. Sababu za kutaka
kutambuliwa huku, ni kuwa kundi hili ni kubwa kuliko hata makundi mengine
yaliyotajwa hapo juu. Takwimu za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2006
zinaonyesha kuwa wasanii nchini walikuwa kiasi cha milioni 6. Leo ni mika
minane imepita na si siri kuwa kundi hili limekuwa na hivyo kukaribia robo ya
Watanzania, si haki kutolitambua.
ii.
Milikibunifu (Intellectual Property) itajwa
rasmi kama moja ya aina za mali zinazohitaji kulindwa katika katika Katiba
Tumekuja pia na mapendekezo ya namna ya kuingiza hoja zetu
hizi zilizosahauliwa, hatujaja na Ibara mpya kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoonekana
kutuhumu katika magazeti ya juzi. Mapendekezo yetu ni kuwa katika Ibara ya 30
iongezwe aya moja tu ya. Na ibara
ya 37 inayoongelea Haki ya ulinzi wa mali, itambue kuwa pamoja na mali
zinazohamishika na zisizohamishika, pia kuna mali isiyoshikika.
Tumepata faraja kubwa kupokelewa na Bunge hili, Na kuweza kuzunguka kwenye kamati 9 kwa
hizi siku mbili kukumbusha mapendekezo yetu haya, ambayo hayabebi tu wasanii
bali pia wavumbuzi wa kiteknolojia, kibailojia, wasomi watafiti, na wananchi
wote kwa ujumla. Pendekezo letu la pili ni muhimu katika kulinda na kuendeleza
uchumi wa Tanzania. Na sisi kama Watanzania tumeona ni muhimu kutumia nafasi
hii adimu kuhakikisha tunatoa mawazo yetu katika Bunge hili kwani tusipotumia
nafasi hii tutakuwa hatukujitendea haki wala kuvitendea haki vizazi vijavyo vya
Tanzania.
SIMON MWAKIFWAMBA-SHIRIKISHOLA FILAMU TANZANIA (TAFF)
JOHN KITIME….MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA (TAMUNET)
Saturday, August 16, 2014
UMUHIMU WA MILIKIBUNIFU KUTAJWA KATIKA KATIBA MPYA
Katika Rasimu ya Katiba kumetajwa ulinzi wa mali, lakini ni wazi mali
hizi ni zile zililzozoeleka katika akili za watu mali zinazohamishika na
zisizohamishika. Kuna aina ya tatu ya mali ni ile inayotokana na
ubunifu, na kwa sasa ndio mali inayolindwa zaidi na mataifa mengi, kwani
ndio inayoleta ugunduzi wa madawa, mitambo, teknolojia, sanaa, na
maendeleo ya kila aina. Hii huitwa Milikibunifu. Ni muhimu kutajwa kama
zilivyofanya nchi nyingine ambazo zimefaidika sana na kulinda
milikibunifu za wananchi wake.....
Milikibunifu au Intellectual Property Rights ni haki
anazopewa mbunifu ili kulinda hali za mali yake ambayo haishikiki. Mali hii
iyokanayo na ubunifu ni muhimu kuilinda kwani matokeo ya mali hii huwa faida
kubwa kwa jamii. Milikibunifu ndizo haki ambazo huwalinda wagunduzi wa
maendeleo katika teknolojia, madawa ya binadamu mifugo na kilimo, njia
mbalimbali za kuongeza ubora na ufanisi wa teknolojia. Milikibunifu imegawanywa
katika makundi mbalimbali ya ulinzi;
i.
Patent – (Hataza) hii ni njia ya kulinda na kusajili
uvumbuzi mbalimbali wa kiteknolojia. Mfano vifaa vya kuvunia mazao kwa haraka
zaidi, au kulima kwa haraka zaidi, vifaa vya uvuvi wa haraka, vifaa vya
mawasiliano na vifaa vyovyote ambavyo vitaongeza thamani ya maisha yetu. Katika
nchi kama Korea ya Kusini ulinzi wa Milikibunifu uliwekwa katika Katiba kuanzia
baada ya vita ya pili ya dunia kwa kufusts mfumo wa Katiba ya Marekani na ulinzi huo umeifanya wananchi wake
ambao ni wabunifu kuweza kuja naubunifu ambao unatikisa dunia vifaa kama
Samsung, Daewoo, KIA, LG ni matokeo ya ulinzi wa kikatiba wa wa Milikibunifu
ii.
Trademarks – (Alama za Biashara ) Alama za
biashara huweza kufikia hatua ambapo zikawa na thamani kubwa kwani huweza
kuaminika. Ili kulinda zisitumiwe hovyo au hata kuibiwa na wenye uwezo zaidi
hulindwa na sheria za kulinda alama hizi. Kwa mfano Cocacola, Vodacom, Dell, na
hapa kwetu Azam, ni majina ya bidhaa ambazo zina aminika, na hivyo kuwa na
dhamani kubwa japo hazishikiki, nazo ni sehemu ya mali ambazo hazishikiki lakini zina thamani
kubwa
iii.
Industrial designs – Hizi ni haki wanazopewa
wale wenye ubunifu wa kuweza kufanya usanii wenye kuboresha muonekano wa kitu
ambacho tayari kimeshagunduliwa. Kwa mfano kila mtu ana simu ya mkononi lakini
muonekano wa simu mbalimbali shape nap engine hali ya kuwa ni ya ku slide au
kufungua au kupokea moja kwa moja ni matokeo ya design, pia vitu kama design za
nguo, viatu , kiti ulichokalia makochi magari, vyote hivyo ndivyo matokeo ya
industrial designs. Kazi za ubunifu huo ni muhimu kulindwa kwani huwa na
thamani kubwa sana, kwa mbunifu na kwa mchango wake kwa nchi.
iv.
Geographical Indication – Huu ni utambulisho wa
wapi chanzo cha mali husika. Kwa mfano mvinyo kutoka Dodoma, Dodoma Wine ni
mzuri na hivyo huitwa Dodoma Wine bila kulinda hili, watu watachukua mvinyo huu
na kuupa hata jina jingine ukaitwa South African wine na hivyo kuiba haki
wanazostaili kupata wakulima wa Dodoma, kutambuliwa kwa jina hili kutasababisha
kutakiwa zaidi kwa wine hii duniani na hivyo kuweza kufanya hata Dodoma kuwa
Wine City jambo ambalo linawezekana lakini nchi haijatambua umuhimu huu. Pia
kuna mchele wa Kyela, Dagaa wa Kigoma na vitu kama hivi ambavyo havipatikani
popote duniani kasoro sehemu iliyotajwa.
Nchi kama Uswiss imejenga jina miaka mingi ya utengenezaji wa saa bora
hivyo saa ikiandikwa Swiss made huwa inajulikana ni bora na huwa gharama zaidi,
Sigara kutoka Cuba, Cuban Cigars ni bei kubwa kwani hazipatikani popote kasoro
Cuba, au mvinyo maarufu kama Champagne, ambao hutoka jimbo la Champagne
Ufaransa, umejijengea sifa kubwa duniani na kuwa na bei kubwa sana kiasi cha
kwamba si rahisi kwa mtu wa kipato cha kawaida kununua. Harusi zetu hutumia
Sparkling Wine na kuiita Shampeni.
v.
Hakimiliki na Hakishiriki – Hizi ni haki
zinazolinda kazi za kisayansi na kisanii. Computer Programs, Data, Utunzi wa
vitabu, miswaada, hotuba, uchoraji, muziki, kazi za usonara, picha za mnato na
filamu, uchongaji na kadhalika. Kazi hizi zimekuwa ni chanzo cha utajiri mkubwa
kwa watu binafsi na Mataifa. Katika nchi ya Marekani kazi za Hakimiliki na
Hakishiriki ni za pili katika uchangiaji wa pato la Taifa. Ripoti ya WIPO ya
2010 ilionyesha kuwa katika nchi ya Tanzania kazi za hakimiliki na Hakishiriki
zilichangia asilimia 4.3 ya pato la taifa, karibu mara mbili ya mchango wa
Madini!. Katika mwaka 2009 kazi za hakimiliki zilitengenza aslimia 5.63 ya
ajira nchini, ikiwa juu ya mchango wa Afya (4.23), Biashara na mambo ya Fedha
Real estate, &Business Service(2.37), Ujenzi (1.38),Usafirishaji na
Mawasiliano (0.92), Umeme, Gas na maji (0.91), Madini (0.89)
Pamoja na umuhimu huu, Katiba
inataja mali zinazoshikika tu-Zinazohamishika na zisizohamishika, hivyo mali
hizi ambazo zimeonyesha kuleta maendeleo makubwa kwa nchi ambazo wakati wa
Uhuru tulikuwa sawa kwa mfano Thailand, India, Malasia, Korea kusini ambazo
zote zimetuacha mbali ni kwa ajili ya ulinzi wa mali hizi zisizoshikika ambazo
ndizo pia zinawezesha mazingira ya kuingiza fedha nyingi za uwekezaji kutoka
kwa wenye pesa na kuanzisha viwanda vyenye mali ya asili ya hapa. Nchi zote
zinazoendelea ambazo ziliwahi kuona umuhimu wa kuweka kipengele cha miliki
bunifu katika Katiba yake mapema, zimeweza kupata maendeleo ya haraka kama
nilivyotaja hapo juu.
Mifano ya nchi nyingine….
Marikani ni nchi moja wapo ambapo ulinzi wa Milikibunifu
umewezesha maendeleo makubwa katika sanaa na teknolojia,
·
U.S. Constitution. Article I, Section 8
provides: "The Congress shall have Power … To promote the Progress of
Science and useful Arts, by securing for limited Times to Authors and Inventors
the exclusive Right to their respective Writings and Discoveries."
·
The Constitution of Malaysia, which is the
supreme law of Malaysia, was adopted on 31 August 1957. Since then, the
Constitution has been amended many times, most recently in 2009.
The Constitution contains provisions on intellectual property.
In the Legislative Lists (List I-Federal List) of the Ninth Schedule, the Constitution gives the federal government the power to enact laws relating to patents, designs, inventions, trade marks and mercantile marks, copyrights (Section 8 (e)).
The Constitution contains provisions on intellectual property.
In the Legislative Lists (List I-Federal List) of the Ninth Schedule, the Constitution gives the federal government the power to enact laws relating to patents, designs, inventions, trade marks and mercantile marks, copyrights (Section 8 (e)).
·
Article 22 ya Katiba ya South Korea inasema (1)
All citizens shall enjoy freedom of learning and the arts. (2) The rights of
authors, inventors, scientists, engineers, and artists shall be protected by
Act
Thursday, July 10, 2014
MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA, AFUNDISHA WAALIMU WA NURSERY MUZIKI
Ili kupata kizazi kitakachoweza kupenda muziki na kutumia vifaa vya muziki ni vizuri kuhakikisha unapata waalimu bora wa muziki. Na ni vizuri kuanza kufundisha watoto wakati wakiwa bado wadogo. Kufanikisha hili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania-John Kitime, akishirikiana na Chuo cha Montesori cha Waalimu wa Shule za Nursery, wameanza mpango wa kuwawezesha waalimu kujifunza japo chombo kimoja cha muziki, na pia njia rahisi za kutunga nyimbo za watoto. Waalimu wanafunzi watarekodi nyimbo walizotayarisha na kuondoka nazo baada ya kumaliza masomo ili waweze kuzitumia kufundishia wanafunzi kwenye vituo vyao.
Thursday, June 19, 2014
COSOTA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA
Rob Hooijer |
CHAMA
cha Hakimiliki cha Tanzania kimekuwa katika wiki moja na nusu ya warsha, na
mikutano ya kukiboresha ambayo inaendeshwa na mtaalamu Robert Hooijer kutoka
Afrika ya Kusini. Kazi kubwa iliyokuwa inafanyika ni kuiwezesha COSOTA kufanya
kazi katika mifumo ya kisasa ya ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha. Mr Hooijer
ni mtu mwenye uzoefu wa miaka mingi katika shughuli za Hakimiliki, aliwahi kuwa
CEO wa CISAC, ambacho ndicho muungano wa vyama vyote vya ukusanyaji mirabaha
duniani na pia alikuwa CEO wa South African Musicians Rights Organisation
(SAMRO) ambayo ndicho chama kikubwa kuliko vyote cha ukusanyaji wa mirabaha
Afrika. Kwa kipindi hiki amekuwa Kenya akisaidia shughuli kama hii na mafanikio
makubwa yamewezekana huko.
WASANII WAKUTANA NA KUTOA MCHANGO KATIKA UTAYARISHAJI WA SERA YA MILIKIBUNIFU YA TANZANIA
Wasanii kadhaa
wakiwemo viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa yote yaliyopo,wiki iliyopita walikutana katika
ukumbi wa Chichi Hotel Kinondoni kutoa mchango wao katika utengenezaji wa Sera
ya Taifa ya Milikibunifu (National Intellectual Property Policy). Katika mradi huu wa pamoja wa Tanzania Musicians
Network (TAMUNET) na Tanzania Film Federation (TAFF), ambao umefadhiliwa na
BEST AC, wasanii hawa walipata nafasi kuchangia mambo mbalimbali kuhusu kipengele cha
Hakimiliki katika sera ya Milikibunifu. Washiriki wakiongozwa na mtaalamu
Ernest Omalla na John Kitime , Mwenyekiti wa TAMUNET na wataalamu kutoka Wizara
ya Viwanda na Biashara, mambo mengi yalipendekezwa yawemo katika sera hiyo.Bado
zinatafutwa taratibu za kuweza kuwapata wadau wengine wa Hakimiliki ili waweze
kuongeza ubora wa sera hii.
ARTISTS HOLD A STAKEHOLDERS MEET ON PROPOSED INTELLECTUAL PROPERTY POLICY
The Ministry of Industry and Trade is in the last phase of preparing the National Intellectual Property Policy. The Policy has been in preparation since 2012. A few days ago artists brought together by Tanzania Musicians Network and Tanzania Film Federation with the help of a grant from Best AC, gathered at the Chichi Hotel in Kinondoni and spent hours coming up with suggestions for the Copyright section of the Policy. Present at the meeting were leaders and members of all the four Federations of Artists and the Tanzania Musicians Network (TAMUNET), also present were officials from the Ministry of Industry and Trade. Tanzania Musicians Network will work with Tanzania Film Federation in collecting all the suggestions of the artists together with other Copyright stakeholders and together come up with a workable Copyright policy for presentation to the Government.
Subscribe to:
Posts (Atom)