Wasanii kadhaa
wakiwemo viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa yote yaliyopo,wiki iliyopita walikutana katika
ukumbi wa Chichi Hotel Kinondoni kutoa mchango wao katika utengenezaji wa Sera
ya Taifa ya Milikibunifu (National Intellectual Property Policy). Katika mradi huu wa pamoja wa Tanzania Musicians
Network (TAMUNET) na Tanzania Film Federation (TAFF), ambao umefadhiliwa na
BEST AC, wasanii hawa walipata nafasi kuchangia mambo mbalimbali kuhusu kipengele cha
Hakimiliki katika sera ya Milikibunifu. Washiriki wakiongozwa na mtaalamu
Ernest Omalla na John Kitime , Mwenyekiti wa TAMUNET na wataalamu kutoka Wizara
ya Viwanda na Biashara, mambo mengi yalipendekezwa yawemo katika sera hiyo.Bado
zinatafutwa taratibu za kuweza kuwapata wadau wengine wa Hakimiliki ili waweze
kuongeza ubora wa sera hii.
No comments:
Post a Comment