MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA umepata ufadhili kutoka
Business Environment Strengthening of Tanzania (BEST – AC) ili kuweza kufanya
utafiti wa kina kupata ukweli wa hali halisi ya ukusanyaji na ugawaji wa
mirabaha ya muziki unaofanywa na COSOTA, na baada ya hapo kutoa ushauri wa nini
kifanyike ili kuboresha hali iliyopo. Madhumuni ya mradi huu ni kuwezesha
kufanya mabadiliko katika tasnia ya muziki ambayo yatatengeneza nafasi za ajira
zenye tija ili kuwezesha tasnia kutoa mchango wake katika pato la Taifa, na
kukuza sifa ya nchi kutokana na wasanii wengi wenye sifa waliomo hapa nchini.
Mradi utaangalia sheria zilizopo zinazohusu ugawaji wa
mirabaha ya wanamuziki na mambo mengine yote yanayohusiana na shughuli ya
ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha na kupendekeza taratibu za kuboresha hali.
Kamati za fedha na utawala zitaanza kazi wiki hii ili
kuweza kufanikisha zoezi hili ambalo linatakiwa likamilike katika muda wa mwezi
mmoja. Wanamuziki watashirikishwa katika semina ambayo itafanyika katika wiki chache zijazo. Mtafiti kutoka Afrika ya Kusini amekwisha ingia mkataba na Mtandao ili
kufanya kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment