Sunday, October 15, 2017
Saturday, October 14, 2017
TANZANIA WOMEN'S BANK YASHIRIKI KIKAMILIFU SIKU YA VICOBA TANZANIA
Banda la TWB au Tanzania Women's Bank lilikuwa moja ya mabanda ambayo yalikuwa mstari wa mbele kuhusu kutoa elimu stahiki kwa watumiaji wa benki hiyo katika siku hii ya Vicoba Tanzania. Vijana wachangamfu waliokuweko katika banda hili walikuwa tayari kutoa elimu yoyote ambayo mtu alitaka kupata kuhusu shughuli ya benki hii ya wote.
Sunday, July 16, 2017
RATIBA YA MSIBA WA MKE WA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO
Mke wa mheshimiwa Waziri wa habari Utamaduni na Michezo, Dr Harrison Mwakyembe, Bi Linah Mwakyembe amefariki usiku wa kuamkia jana Jumapili, katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam alikokuwa anatibiwa. Ratiba ya msiba ni kama ifuatavyo:
Jumanne 18/7/2017 asubuhi mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwa Mhe. Dr Mwakyembe Kunduchi Beach, kisha taratibu za Ibada na kuaga zitafuata na hatimae mwili kusafirishwa kwenda Kyela zitafanyika siku hiyohiyo. Mazishi yatakuwa Kyela siku ya Jumatano
Mungu Amlaze Pema Linnah Mwakyembe

Wednesday, June 21, 2017
MTANDAO WA MUZIKI TAMUNET WAJIPANGA UPYA
Katika kuadhimisha Siku ya Muziki Duniani ambayo husherehekewa kila tarehe 21 June, wajumbe wa Mtandao wa Muziki, Tanzania Musicians Network, leo wamesherehekea kwa kufanya kikao kilichojenga kamati ya uongozi ya mud, viongozi hawa watakuwa katika uongozi kwa mwaka mmoja kisha kutayarisha Mkutano Mkuu wa kuchagua viongozi wa kudumu. Katika kikao cha leo kilichotumia masaa matatu safu ya uongozi mpya ni kama ifuatayo;
1. Mwenyekiti - John F Kitime
2. Makamu Mwenyekiti - Rashid Pembe
3. Katibu Mkuu - Innocent Nganyagwa
4. Katibu Mkuu Msaidizi - Geophrey Kumburu
5. Mweka Hazina - Asha Warsama
6. Wajumbe - David Ng'asi, Abdul Salvador
TAMUNET ni chama ambacho malengo yake ni kutetea haki za wanachama wake kama wafanyakazi katika tasnia, na kuwa chama rasmi cha wafanyakazi waliomo katika tasnia ya muziki (Musicians Union). Uongozi uliopo unajipanga kuhakikisha chama kinafanya kazi yake ambayo imo katika katiba yake.

Picha za uongozi mpya wakiwa katika kikao
Wednesday, June 14, 2017
Friday, April 7, 2017
MWANAMUZIKI UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA FETE DE LA MUSIQUE?
Haya
tena wanamuziki wenzangu tamasha la Fête de la Musique
linawakaribisha wanamuziki wa kila aina kuomba kushiriki katika msimu wa sita
wa tamasha litakalofanyika tarehe 17 mwezi juni 2017 Johannesburg, South
Africa. Mwisho wa kupelka maombi ni Ijumaa tarehe 28 April 2017.
Namna ya kuomba
Wasanii wanaotaka kushiriki wapeleke
maombi yao yakiambatana na :
·
Maelezo ya historia ya msanii (Artist biography)
·
Picha
(Photo)
- Maelezo ya kiufundi ya vifaa utavyotumia jukwaani (Technical rider)
- Nakala ya muziki wako (Sound clips)
- Videos
- Maelezo yako yatakayoweza kutumika katika matangazo (Press kit)
Maombi
yote yanaweza kutumwa kupitia fetedelamusiquejoburg@gmail.com wakati
fomu za maombi zinapatikana HAPA
Fête
de la Musique ni tamasha ambalo linaweza kuhudhuriwa na familia nzima bila
kujali rika, nia yake ikiwa ni kufurahia muziki wa’live’. Pia ni mahala ambapo
wasanii kutoka nchi mbalimbali wanaweza kukutana.
Kwa
kuwa kuna maelfu ya wapenzi wa muziki hukutana hapa katika tukio hilo la mara
moja kwa mwaka, wanamuziki maarufu na wasio maarufu hupanda jukwaa moja.
Tamasha lipo kwa hisani ya Alliance Francaise Johannesburg na French Institute
of South Africa, wakishirikiana na Bassline Live kwa ufadhili wa Total.
Mwaka
2016, Fête de la Musique iliwakusanya
karibu watu 8 000 katika mji wa Newtown, Johannesburg. Baadhi ya wasanii
walioshiriki walikuwa Vaudou
Game (France), Blk Jks
(South Africa), Les Fantastiques (DRC), Jess & Crabbe (France), Bombshelter
Beast (South Africa), Mapumba Cilombo (DRC), Morayks (Lesotho), Zanmari Baré
(Reunion Island) na wengine wengi.
Wednesday, March 29, 2017
UNATAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA SANAA UGANDA?
JE, unataka kushiriki katika tamasha la Bayimba
International Festival, ambalo litafanyika tarehe 15-17 September 2017 Kampala, Uganda?
Tamasha la
mwaka huu litakuwa ni la kumi. Ni tamasha ambalo linajumuisha muziki, dansa,
maonyesho jukwaani, filamu, vichekesho, mashahiri, na sanaa za maonyesho.
Wanaohitaji kushiriki ni muhimu kuwa wameshajaza fomu zao na kutuma ifikapo
April 30. Katika tamasha la mwaka jana walikuweko wasanii wa Hiphop kama Akua Naru kutoka Ghana, Tribute
‘Birdie’ Mboweni toka Afrika ya kusini, bibie wa Kiganda ambae ni mpiga
saxaphone wa mahadhi ya soul Mo Roots, kundi la Reggae toka Kenya Gravittii
Band, na wengine wengi. Kutakuwepo na malipo kidogo kwa washiriki toka nje ya
Uganda, japo washiriki wanashauriwa kutafuta njia za kulipia gharama za
usafiri, viza na bima mbalimbali. Barua ya utambulisho itatolewa mara
utakapokubaliwa kushiriki ili ikusaidie kutafuta ufadhili. Wanaotaka kushiriki
wanatakiwa watoe taarifa zifuatazo,
·
Fomu ya
ushiriki na kupitia bayimbafestival.com
·
Maelezo mafupi ya wasanii yasiyozidi maneno 800 na
picha ya karibuni
·
Nakala ya kazi yako, kama ni muziki au filamu kazi
moja au mbili kwenye CD, DVD or mp3.
·
Mahitaji yako ya vifaa (technical rider/data sheet)
Watayarishaji
watawajibu mapema waliofanikiwa.Fomu za maombi zinapatikana pia HAPA
Saturday, November 26, 2016
CDEA WAZINDUA MRADI WA ATAMISHI YA KAZI ZA SANAA ‘IIDEA’ KUSAIDIA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA) leo limezindua rasmi mradi wa Atamishi ya kazi za sanaa (IIDEA) ambapo utakuwa nguzo muhimu kwa nchi za Umoja Wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye, ameeleza kuwa sanaa ni ajira hivyo mpango huo utasaidia kuinua ajira kwa wasanii watakaofikiwa na kukuza soko la Afrika Mashariki kupitia Sanaa zao.
“Sanaa ni kazi ya kujikimu na kazi ni hutu hivyo ni wajibu wa kila msanii kujiheshimu na kufuata taratibu ili kuwa njia kwa jamii na kuheshimika zaidi hasa katika sanaa yake. Nawapongeza sana CDEA kwa mpango huu kwani utaendelea kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, utasaidia Wasanii wetu kupanua mawazo yao zaidi na kujiongezea maarifa ya juu katika taaluma yao ya Sanaa.” Alieleza Bw. Habibu Msammy.
Pia alisisitiza kuwa mafunzo watakayoyapata wayatumie kujiimalisha kiuchumi huku akisisitiza kuwa bado wanayo nafasi ya kujifunza zaidi katika kuweza kubuni vazi la Taifa.
“Kwa kuwa mradi huu unagusa sanaa za Ubunifu wa mavazi, Urembo na filamu. Wabunifu wa Tanzania ni wasaha wa kuendelea kubuni vazi la Taifa, Wasanii wanaangaliwa na wengi hivyo kuanzia mavazi na mawazo yao ya ubunifu na tunawategemea pia katika kubuni vazi letu la Taifa” alieleza Habibu Msammy.
Mradi huo wa mwaka mmoja unatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa wabunifu wa mavazi na urembo, Wanamuziki na wasanii wa filamu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa amebainisha kuwa, baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa wataanza mchakato wa kupata washiriki ambapo wahusika watatakiwa kutuma maombi ya ushiriki baada ya kuona matangazo mbalimbali yatakayotolewa na CDEA kupitia mitandao ya kijamii na sehemu zingine za Utamaduni.
Katika uzinduzi huo, watu mbalimbali wameshiriki wakiwemo wasanii wa filamu, maigizo, wabunifu wa mavazi, wanahabari, wanamuziki na wasanii wa kazi za sanaa ikiwemo za mikono na ubunifu.
Afisa wa Mradi wa IIDEA, Bi. Angela Kilusungu wa CDEA, akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo mpya wa utakaosaidia sanaa kwa Afrika Mashariki
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya CDEA, wakiwa katika mkutano huo
Allen Enjewele wa CDEA akifanya mahojiano katika tukio hilo
Msanii Remigius Sostenes wa CDEA akitoa burudani katika tukio hilo
Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akijadiliana jambo na Mjumbe wa bodi hiyo ambaye anatokea Burundi, Bw. Gilbert Hagabimana wakati wa uzinduzo huo.
Baadhi ya wadau wa Sanaa nchini wakijadiliana katika uzinduzi huo
Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa (kushoto) akijadiliana jambo na wadau wa sanaa
Msanii Nick wa Pili akielezea namna sanaa inavyohitaji ubunifu wakati wa tukio hilo
Baadhi ya wadau wa sanaa na wanahabari wakipata kujadiliana jambo
Wadau wa sanaa wakifuatilia makala fupi ya CDEA iliyokuwa maalum wakati wa uzinduzi huo
Uzinduzi huo ukiendelea
Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa akielezea jambo katika tukio hilo
Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akitoa neno na kumkaribisha mgeni rasmi
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua rasmi mradi huo
Mzee Kitime mmoja wa wadau wa Sanaa nchini akifuatilia kwa makini tukio hilo la uzinduzi
Wadau wa kifuatilia uzinduzi huo
Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya uzinduzi wa mradi huo wa IIDEA, mapema leo Novemba 25.2016.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE
Tuesday, November 22, 2016
Mkataba wa Kumkodi Mwanamuziki au Mwimbaji Msindikizaji Kwa ajili ya kurekodi
Ni jambo la kawaida kabisa kuona makubaliano makubwa katika tasnia ya muziki Tanzania yanafanywa bila mikataba bali kwa makubaliano ya mdomo. Hili ni tatizo ambalo lazima lirekebishwe, kwani linaleta hasara kubwa kwa wasanii kutokupata haki zao stahili na mara nyingine kudhulumiwa kabisa. Hivyo basi kwa kuwa mikataba ya muziki huwa na lugha ngumu ifuatayo ni mikataba mabayo imerahisishwa na UNESCO ili wanamuziki waweze kuitumia kwa marekibisho kidogo kutegemeana na hali halisi. Hii ni mifano ya mikataba ambayo hutumika dunia nzima. Usikubali kuanza kazi bila mkataba wa maandishi….
JE UNATAKIWA KUFANYA KAZI YA MUZIKI KWENYE ALBUM YA MTU MWINGINE?
MKATABA HUU HAPA
Mkataba unaeleza masharti ya kumkodi mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji kwa ajili ya kurekodi santuri moja au zaidi zitakazotayarishwa kibiashara. Mkataba unaainisha wajibu wa mtayarishaji na vilevile ule wa wanamuziki na waimbaji.
MWANAMUZIKI AU MWIMBAJI MSINDIKIZAJI MTAYARISHAJI WA SANTURI
KIFUNGU CHA 1 – Madhumuni.
Mtayarishaji anamkodi mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji katika nafasi yake ya kitaalamu kurekodi santuri moja au kadhaa. Santuri zitatumiwa mojamoja au kama sehemu ya Albamu. Mkataba lazima ujazwe kikamilifu pale inapobidi, kwa kuzigatia masharti ya sheria za kazi za nchi ambazo mkataba unasainiwa.
KIFUNGU CHA 2 – uidhinishaji wa Matumizi. MWANAMUZIKi au MWIMBAJI MSINDIKIZAJI anaidhinisha upangiliaji wa maonesho yake na kurudufu santuri zilizoainishwa kwenye kifungu cha 1 na vile vile kufanya biashara ya santuri hizo kwa umma. Hivyo mtayarishaji atakuwa na haki ya kuzalisha, kuchapisha, kusambaza itakuvyokuwa kuuza kwenye kibebeo cha aina yoyote ( K7, CD, DVD ya sauti au muundo wowote wa siku zijazo nk ) au kwa mawasiliano ya mtandao (Intaneti na mingineyo), kutangaza katika muundo wowote, chini ya kichwa cha habari, nembo au alama ya chaguo lake na duniani kote, santuri zilizoanishwa katika kifungu cha 1. Unufaikaji wowote zaidi ya matumizi yaliyoelezwa hapo juu, yakiwamo matumizi kwa ajili ya matangazo ya biashara, matumizi ya kielimu, matumizi katika sinema au onesho, na matumizi kwenye bidhaa maalumu, yatahitaji kwanza kupata idhini ya asasi ya usimamizi wa pamoja inayosimamia haki za wanamuziki na waimbaji wasindikizaji. Ili kuruhusu matumizi sahihi ya haki. Mtayarishaji anawajibika kuhakikisha mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji anasaini karatasi ya kurekodi kipindi kulingana na taratibu za kitaalamu, na kuwasilisha nakala ya karatasi hii ya kurekodi kipindi kwenye asasi ya usimamizi wa pamoja ambayo inasimamia haki za wanamuziki na waimbaji wasindikizaji katika nchi zilizotarishwa santuri. Zaidi ya hayo msanii anaridhia matumizi ya jina na picha yake, kama vitahitajika, kuhusiana na matumizi ya santuri hizo.
KIFUNGU CHA 3 – Wajibu wa mtayarishaji. MTAYARISHAJI anajukumu la kuheshimu wajibu wote uliowekwa na sheria za kijamii kuhusiana na kumkodi MWANAMUZIKI au MWIMBAJI MSINDIKIZAJI. Mtayarishaji anawajibika kumlipa mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji kiasi cha _____________________ kwa kila kipindi cha kurekodi, ili kufidia kushiriki kwake katika kurekodi santuri, na vilevile kwa ajili ya uchapishaji na mauzo ya miziki kwenye aina yoyote ya kibebeo (K7, CD, DVD ya sauti n.k) au katika mawasiliano ya mitandao (Intaneti au mingineyo). Upigaji wa santuri katika utangazaji utatakiwa kuliipiwa moja kwa moja na mashirika ya utangazaji kwenye asasi ya usimamizi wa pamoja ambayo inasimamia haki za wanamuziki na waimbaji wasindikizaji katika nchi matangazo yanamotolewa.
KIFUNGU CHA 4 – wajibu wa Mwanamuziki au Mwimbaji Msindikizaji.
Mwanamuziki kutoka nje au mwimbaji msindikizaji kutoka nje ya nchi anahakikisha kuwa amepewa kibali cha kufanya kazi kwenye nchi santuri zinapotayarishwa na kuwasilisha uthibitisho wa jambo hilo. Mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji anawajibika kuwepo kuanzia ___________________ hadi
___________________katika sehemu ifuatayo _____________________ kushiliki katika vipindi vya kurekodi ambavyo vitafanyika kulingana na ratiba zifuatazo:- ______________________________________________________________________________ Kifungu cha 5 – mambo mbalimbali
Mkataba huu unaongozwa na sheria ya nchi unamofanyika utayarishaji.
Umesainiwa (mji)…………………………………….. Tarehe ……………….. Katika ……………… nakala halisi.
MWANAMUZIKI AU MWIMBAJI MSINDIKIZAJI ________________________________________________________________________ MTAYARISHAJI ________________________________________________________________________
Mkataba wa kumkodi Mwanamuziki au
Mwimbaji Msindikizaji
Kwa ajili ya kurekodi
Santuri

Subscribe to:
Posts (Atom)