Msama |
Kitime |
Mtandao wa Muziki Tanzania umempa hongera Msama na kampuni yake ya Msama
Auction Mart
kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiendelea nayo muda mrefu ya kukamata wezi wa kazi za muziki na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kupunguza uharamia na kuhamasisha uchangiaji wa pato la Taifa kupitia kazi za sanaa. Katika pongezi hizo Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime amesema, 'Kwa niaba ya
wanachama wa chama chetu Tanzania Musicians Network, naomba nitoe shukrani kwa
mchango wako mkubwa ambao kampuni yako inaufanya katika jitihada za kupunguza
uharamia wa kazi za sanaa Dar es Salaam.
Tuko tayari kushirikiana nawe kila wakati kwa lengo la kuboresha
mazingira yanayohusu uboreshwaji wa stahiki za wanamuziki wakati wowote.Tunarudia tena kushukuru kwa hili'
Msama amekuwa akifanya kazi hii ya kukamata kazi zisizo halali kwa miaka mingi, na Kitime amekuwa mwanaharakati wa swala la Hakimiliki kwa miaka mingi pia.