MWANAMUZIKI wa Abuja, nchini
Nigeria Omenuwoma Okson Dovie, aka Baba 2010, ameamua kuipeleka mahakamani
kampuni ya simu ya MTN kwa kukiuka
haki zake za hakimiliki katika nyimbo zake nne, zikiwemo "Gentleman
"Ometena", "Twisted" and "Unity Song."
Dovie anaituhumu kampuni
hiyo kwa kubadili nyimbo hizo kuwa caller tunes/ring tones, na kuziuza bila
ruksa yake kwa miaka mitatu mfululizo. Nyimbo hizo ziko kwenye album yake aliyoitoa
2005 ikiwa na jina
"Twisted”.
Barua ya mwanasheria wake
Rockson Igelige, imeitaka MTN
kumlipa mteja wake naira milioni
500 (Tshs 5,455,000,000), kwa matumizi ambayo hayakuruhusiwa na yenye kupunguza thamani ya nyimbo
zake. Na pia alitoa siku 14 ambazo MTN lazima iwe imekamilisha malipo au kujibu
hoja.
Mshauri wa sheria wa MTN
amekubali kuwa kapokea barua na kuwa kampuni hiyo inaliangalia swala hilo.
Wakati huohuo Igelige amesema wameishauri Kamisheni ya Hakimiliki ya Nigeria
kuwafungulia mashtaka MTN, wakati nao wakifungua mashtaka kwa upande wa
mwanamuziki.
No comments:
Post a Comment