The Ministry of Industry and Trade is in the last phase of preparing the National Intellectual Property Policy. The Policy has been in preparation since 2012. A few days ago artists brought together by Tanzania Musicians Network and Tanzania Film Federation with the help of a grant from Best AC, gathered at the Chichi Hotel in Kinondoni and spent hours coming up with suggestions for the Copyright section of the Policy. Present at the meeting were leaders and members of all the four Federations of Artists and the Tanzania Musicians Network (TAMUNET), also present were officials from the Ministry of Industry and Trade. Tanzania Musicians Network will work with Tanzania Film Federation in collecting all the suggestions of the artists together with other Copyright stakeholders and together come up with a workable Copyright policy for presentation to the Government.
Thursday, June 19, 2014
Wednesday, June 18, 2014
TAMUNET WAFANYA MKUTANO NA WANACHAMA
TAMUNET- Mtandao wa Wanamuziki Tanzania umefanya mkutano katika
ofisi za mtandao huo, jirani na Kinondoni Mahakamani, ambao wanamuziki na
viongozi wa bendi walialikwa katika kuongelea changamoto zinazoikabili tasnia
hiyo. Mkutano huo ulianza kwa Mwenyekiti wa Mtandao John Kitime kutoa ripoti ya
utendaji wa Mtandao huo toka ulipoanza na changamoto ambazo Mtandao umepitia.
Baadhi ya mafanikio ya Mtandao huo ni kukamilisha ripoti
iliyofadhiliwa na BEST AC ambapo kwa kutumia mtaalamu kutoka Afrika ya Kusini
waliweza kutengeneza ripoti iliyoitwa
Study on Artists Copyright Management& Royalties Collection and
Distribution in the Tanzania Music Industry. Ripoti hii ilionyesha changamoto
za ukusanyaji na ulipaji wa mirabaha kwa wanamuziki wa Tanzania. Nakala ya utafiti
huu ilikwisha wasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na
Michezo, ili kuwezesha TBC ambayo ni redio na TV ya Taifa kuanza kulipa mirabaha kadri ya maelekezo ya
sheria ya Hakimiliki na hakishiriki. Bahati mbaya mpaka sasa Wizara haija
onyesha ushirikiano kwa hili.
Mtandao pia umeshiriki katika kuwasilisha kwenye Bunge la
katiba mapendekezo makuu ya wasanii, i. Wasanii kutajwa katika Katiba kama kundi maalumu kama
walivyotajwa wakulima, wafugaji na wavuvi, kwa kuwa idadi ya wasnii ni kubwa
sana, wanaingiza kipato kuliko wavuvi, na inaajiri watu wengi kuliko wavuvi.
Pia Mtandao umeluweko katika mchakato wa kutengeneza sera ya Milikibunifu.
Mtandao ni mwananchama wa International Federation of
Musicians na mwenyekiti aliwaasa wanamuziki kutumia fursa zinazotokana na
uanachama wa shirika hilo.
Kikao kilamua kutengeneza kamati ya kukutana na wanamuziki
katika sehemu zao za kazi ili kuongeza wanachama. Na pia kuangalia shughuli za
kijamii ambazo wanamuziki wanaweza kufanya kama mchango wao kwa jamii.
Baada ya chakula cha mchana wajumbe walitawanyika
Tuesday, April 15, 2014
Sunday, April 13, 2014
MAZISHI YA MZEE MUHIDIN GURUMO KUWA KESHO JUMANNE -15/4/2014
Mazishi ya Mzee Gurumo kuwa kesho kijiji alichozaliwa huko Masaki. Mwili wa Mzee Gurumo utaondoka kwake Mabibo kesho asubuhi saa nne kuelekea kwenye Masaki
Tuesday, March 25, 2014
MKUTANO WA KWANZA WA VIONGOZI WA BENDI WAFANYIKA BASATA
Mkutano wa kwanza wa viongozi wa bendi mwaka huu, uliofanyika katika
ukumbi wa Basata Jumanne tarehe 25 March umekuwa na mengi mazuri. Kwanza wanamuziki
walikumbushwa mengi ambayo yameshindikana kufanyika kwa kutokuweko na umoja
wenye nguvu wa wanamuziki, hasa wa muziki ‘live’, hivyo kulipatikana azimio
kuwa wanamuziki wahamasishane wenyewe kujiunga na vyama vya muziki.
Maelezo pia
yalitolewa kuhusu nafasi ya sanaa katika Katiba mpya na juhudi ambazo
zimekwisha fanywa na jinsi zinavyohitaji umoja katika kipindi hiki cha Bunge la
Katiba. Viongozi hawa hatimae walizungumzia changamoto mbalimbali ambazo
zinaikumba tasnia hii, na kuamua kuanza kujipanga kupunguza matatizo yale
ambayo yako katika uwezo wa bendi. Iliamuliwa kuweko na kikao kingine Jumanne
ijayo kuanzia saa nne asubuhi palepale BASATA na kutafuta wajumbe wengine kutoka bandi ambazo hazikuhudhuria mkutano wa leo.
Wednesday, March 5, 2014
MTANDAO KUFANYA WARSHA YA VIONGOZI WA BENDI
Kamati ya uongozi ya Mtandao wa wanamuziki(TAMUNET), leo imefanya kikao na katika yaliyopangwa na kufanya warsha ya siku moja ya viongozi wa bendi kujadili changamoto mbalimbali zinazozikuta bendi katika zama za sasa. Tarehe ya warsha hii inategemea makubaliano na BASATA ambao watakuwa kiungo muhimu katika warsha hii. Lakini warsha hii lazima itakuwa mwezi huu March kabla ya mkutano mkubwa wa wanamuziki mara baada ya warsha hiyo.
Wednesday, February 19, 2014
HARAKATI ZA WASANII KUPATA NAFASI KATIKA KATIBA MPYA—3
Kamati ilipata
mapokezi ya heshima kubwa kutoka kwa wabunge wa CHADEMA, ambapo Wabunge sita wa CHADEMA walikaa na kuwasikiliza
wawakilishi hawa wa wasanii wakieleza mapendekezo yao katika Katiba kuhusiana
na wasanii. Wasanii wana ajenda mbili,
1. Kundi la wasanii kutajwa katika
Katiba kuwa ni kundi rasmi kutokana na ukubwa wa kundi hili nchini, kama yalivyotajwa makundi ya wakulima, wafugaji, wavuvi na kadhalika, pia mchango
wake katika ajira ya vijana na ukubwa wa pato linalotokana na kundi hili,
ambalo kutokana na kutokutambuliwa linapotea katika mifuko ya watu na kukosesha
wasanii na Taifa pato kubwa.
2. Wasanii walitaka ubunifu ulindwe kwanza kwa
ulinzi wa Milikibunifu kutajwa rasmi katika katiba na hivyo kuwezesha sheria bora kutungwa na pia
utekelezaji wa ulinzi wa kazi zao uweko kama ilivyo katika mali nyingine za
wananchi wengine. Kikao cha saa moja na nusu kilikuwa cha mafanikio na kuwa na
faida kwa pande zote mbili.
Wasanii hawakulala mapema kwani walimalizia siku na
kuhamia eneo jingine ambapo
walikuwa na kikao na Mheshimiwa Mbunge wa Donge ambae pia ni Mwenyekiti wa
Ummoja wa Vijana wa CCM Taifa Mheshimiwa Sadifa, ambapo kikao hicho kiliisha saa saba
ya usiku.
HARAKATI ZA WASANII KUPATA NAFASI KATIKA KATIBA MPYA—2
Ili kuwezesha kufika Dodoma na kuwakilisha mapendekezo
yaliyokusanywa na Mashirikisho, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET),
waliwezesha idadi ya wasanii 12 kufika na kuishi Dodoma. Wasanii hao wakiwemo
viongozi toka Mashirikisho wameza kufika Dodoma na kuanza kazi mara moja ya
kukutana na Wabunge mbalimbali, na kufanya nao mikutano na mazungumzo ya papo
kwa popa na kwa kweli mapokezi yamekuwa ya hali ya juu yanayoleta tumaini kubwa
kwa wote waliofika huku. Wasanii
waliomo katika msafara huu muhimu kwa tasnia na Taifa ni
1.
Simon Mwakifwamba – Rais, Shirikisho la Filamu
(TAFF)
2.
John Kitime – Mwenyekiti, Tanzania Musicians
Network (TAMUNET)
3.
Bishop Hiluka – Katibu Mkuu, TAFF
4.
Yobnesh ‘Batuli’ Yusuph –Msanii/FilmProducer
5.
Samwel ‘Braton’ Mbwana –Tanzania Urban Music
Association (TUMA)/Music Producer
6.
Paul ‘P Funk’ Matthysse – Mwenyekiti, Tanzania
Producers Association/ Producer
7.
Kulwa ‘Dude’ Kikumba – Msanii/ Producer
8.
Abdul Salvador –Katibu Mkuu, Shirikisho la
Muziki Tanzania (TMF)
9.
Adrian Nyangamale – Rais, _Shirikisho la Sanaa
za Ufundi Tanzania
10. Mh.
Paulynus Raymond Mtendah – Mbunge Bunge la katiba
11. Yvonne
Cherie ‘Mona Lisa’ –Msanii
12. Seleman
Hamisi- Producer toka Dodoma
13. Ernest
Omalla – Mshauri wa TAFF na TAMUNET
Mara baada ya kufika Dodoma Mbunge wa Bunge la Katiba Mh.
Maria Sarungi aliwezesha kufanyika kikao cha kwanza kati yake na wasanii ambapo
pia Mh. Paul Makonda alikuweko. Mazungumzo yalifanyika ambapo msafara ukaweza
kueleza mapendekezo yake kupitia mshauri mtaalam Ernest Omalla na mwanamuziki
John Kitime. Mkutano huu wa saa mbili ulikuwa wenye matumaini makubwa.
Msafara
ulitoka hapa na kwenda kwenye mkutano mwingine ambapo msafara tena ulitoa
maelekezo yake kwa waheshimia Wabunge watatu, Mh Paul Mtanda, Mh.Livingstone na
Mh Murtaza Mangungu, na tena mkutano huo ulikuwa ni mzuri wenye mafanikio
mazuri sana. Mheshimiwa Mtanda aliahidi atajitahidi kukusanya wajumbe wa kamati
ya Ustawi wa Jamii ili kuweza kupata uelewa wa maombi ya wasanii.
Kamati haikuishia hapo kwani jioni Mheshimiwa Makonda aliiwezesha kundi hili kukutana
na wabunge wengine wakiwemo Mh.
Ahmed Salum, Mh. William Mgeja na Mh. Mpina Mbunge wa Kisesa.
Katika hali ya
kuonyesha kuwajali wasanii wabunge wa Dar es Salaam waliwafuata wasanii katika
Lodge waliofikia na kuwasikiliza lile ambalo walikuwa wakilitaka. Mheshimiwa
Idd Azan na Mh. Abbas Mtemvu waliwakilisha wabunge wa Dar es Salaam na kuwa na
saa nzima ya kuwasikiliza wasanii hawa katika malengo yao
mawili waliyotaka yaingie katika Katiba.
Tuesday, February 18, 2014
HARAKATI ZA WASANII KUPATA NAFASI KATIKA KATIBA MPYA—1
MH. PAULYNUS RAYMOND MTENDA |
Kuna
mashirikisho manne ya sanaa nchini ambayo ni Shirikisho la muziki, Shirikisho
la Filamu, Shirikisho la Sanaa za maonyesho na Shirikisho la Sanaa za Ufundi.
Ulipotolewa wito wa makundi maalumu kutoa mapendekezo yao katika Katiba
Mpya, Mashirikisho yalikaa kama
Kamati za katiba na kuja na mapendekezo kadhaa kwenye katiba, mapendekezo hayo
licha ya kupokelewa na Tume ya Katiba hakuna kilichoingizwa katika Rasimu ya
Katiba.
Baada ya hapa ndipo wito ukatolewa wa kupendekeza majina ya
watu watakaoingia katika Bunge la Katiba, Mashirikisho yote yalipendekeza
majina mbalimbali. Hatimae jina la Paulynus Raymond Mtenda lilirudi kama ndie
mwakilishi aliyeweza kutoka katika kundi la Watu wenye malengo yanayofanana .
Tarehe 14, February 2014 viongozi wa Mashirikisho walikutana
BASATA kumpongeza Mbunge Mteule huyu na kumkabidhi rasmi mapendekezo ambayo
yalipelekwa awali kwenye Tume ya Katiba ili aweze kuyapendekeza katika katiba
mpya.
KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BASATA AKIMKABIDHI MAPENDEKEZO YA MASHIRIKISHO MBUNGE MTEULE |
Pamoja na mapendekezo hayo Shirikisho la Filamu TAFF, na
Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET), pia walikuja na hoja mbili muhimu
nazo ni;
1.
Kutambuliwa kwa wasanii kama ni kundi maalumu katika
Katiba, kama yalivyoweza kutambuliwa makundi ya wakulima, wavuvi na
wafanyakazi. Sababu kubwa za kuja na hoja hii ni kutokana na ukweli
unaopatikana katika tafiti mbalimbali.
Wasanii ni wengi sana, katika ripoti ya BASATA ya mwaka 2006, idadi ya
wasanii nchini wakati huo ilikuwa kiasi cha milioni sita. Kwa kuwa ni miaka
minane sasa imepita toka wakati wa ripoti hiyo kuna kila sababu ya kuamini kuwa
kundi hilo limekuwa kubwa zaidi. Sababu nyingine ni ukweli kuwa wasanii
wanasababisha ajira kwa kundi kubwa la watu, wakiwemo wafanyakazi wa vyombo vya
utangazaji, wafanya kazi katika biashara ya matangazo, wasambazaji, wafanya
biashara ndogondogo, (machinga) na wengine wengi waliomo katika mnyororo wa
biashara hii ikiwemo, maproducer, mameneja, mafundi mitambo, watayarishaji wa
maonyesho na kadhalika. Hivyo sanaa si utamaduni tu bali ni kazi yenye mapato
makubwa. Ripoti ya WIPO ya mwaka 2012 imeonyesha kuwa kazi zitokanazo na
Hakimiliki huingiza fedha nyingi zaidi katika uchumi wa Taifa kuliko MADINI,
jambo ambalo ni wazi wengi wanaosikia kwa mara ya kwanza hushangaa kwa kuwa
kelele za mapato ya Madini ni kubwa sana katika jamii wakati hakuna
anaelalamika kuhusu mapato kutokana na hii raslimali ya nchi inayoitwa sanaa.
Ripoti hiyo ya WIPO pia ilionyesha kuwa sekta ya Hakimiliki inaajiri watu wengi
zaidi kuliko, sekta za Madini, gesi, maji, Ustawi wa Jamii, Afya, Usafirishaji.
Hivyo ni sekta ambayo ina umuhimu sana katika uchumi wa Taifa ikiwa italindwa inavyostahili.
2.
Hoja ya pili ilikuwa kuwekwa rasmi kipengele cha
kutambuliwa kwa Miliki Bunifu na kuhakikishiwa ulinzi na uendelezaji wa
shughuli za Milikibunifu katika Katiba. Wasanii hutegemea maendeleo yao na
uboreshaji wa kazi zao kwa kulindwa kwa Hakimiliki. Lakini ingekuwa ni uchongo
wa mawazo kudai ulinzi wa Hakimiliki peke yake. Hivyo lengo ni kupata ulinzi wa
Miliki Bunifu ambayo itasababisha kulinda haki za wasanii ,wabunifu, wagunduzi,
wanasayansi na wabunifu wa teknolojia mbalimbali. Kuna mifano kila mara hutolewa ambayo
inaonyesha nchi kadhaa ambazo wakati nchi hii inapata uhuru, uchumi wa nchi
hizo ulikuwa sawa na uchumi wetu, kama vile Malasia, Thailand na Korea Kusini ambazo
kutokana na ulinzi na uendelezaji
wenye mipango wa Miliki Bunifu nchi hizo zimewezesha uchumi wao kukua na kuwa katika
uchumi bora duniani.
Subscribe to:
Posts (Atom)