Katika Jukwaa la Sanaa ambalo huweko kila Jumatatu katika ukumbi wa BASATA , wiki hii Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki John Kitime alichambua utafiti uliokamilika karibuni uliofanywa na mtafiti Martin Cuff kwa niaba ya Mtandao kwa ufadhili wa BEST AC. Utafiti huo ambao umo kwenye kitabu chenye kurasa 84 unachambua hali halisi ya Hakimiliki Tanzania, na mapungufu yake na kisha kutoa mapendekezo ya kuboresha hali hiyo kwa manufaa ya wenye Hakimiliki na tasnia ya muziki kwa ujumla. Kitabu cha utafiti huo kitapatikana baada ya muda si mrefu.
Wednesday, November 20, 2013
Thursday, November 7, 2013
UBALOZI WA MAREKANI WAKABIDHI VITABU 800 KWA MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA
Ubalozi wa marekani nchini Tanzania, leo hii 7/11/2013
umemkabidhi vitabu vya Hakimiliki zaidi ya 800 Mwenyekiti wa Tanzania
Musicians Network, John F Kitime katika hafla iliyofanyika katika maktaba ya
Ubalozi huo uliopo jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho chenye lugha mbili
Kiswahili na Kiingereza kimetungwa na Alex Perullo ambaye ni Associate Professor wa Anthropology na African Studieskatika chuo cha
Bryant Marekani. Hiki ni kitabu cha pili cha aina hii kutungwa na Profesa huyu,
cha kwanza alikisambaza kupitia Ubalozi huu huu miaka kumi iliyopita. Kwa vile
kina lugha mbili kitabu hiki kina majina mawili kinaitwa Artistic Rights na
Haki za Kisanii. Ni kitabu cha kurasa 98 ambacho kimejaa maelezo mengi kuhusu
haki za wasanii, wasanii watakao kisoma watafaidika sana.
Mtandao wa Muziki Tanzania, utakisambaza
kitabu hiki katika taasisi mbalimbali muhimu na pia utawapa bure wanachama wake
nakala za kitabu hiki muhimu. Dibaji ya kitabu hiki imeandikwa na John Kitime.
Subscribe to:
Posts (Atom)