Tuesday, May 28, 2013
SOMA GAZETI LA INTERNATIONAL FEDERATION OF MUSICIANS HAPA
INGIA HAPA KUSOMA GAZETI LA INTERNATIONAL FEDERATION OF MUSICIAN BONYEZA
Tanzania Musicians Network chaanza upya kwa kishindo
-->
Tanzania Musicians Network au Mtandao wa Wanamuziki Tanzania ni chombo
kilichosajiliwa BASATA 2004,
kilianza kwa nguvu mwaka 2006 na kufikia kuwa na wanachama 400, lakini kilipata pigo mwaka 2007 kwa jengo
ambalo lilikuwa ofisi ya chama hiki kuvunjwa na kulibadilishwa matumizi na
mwenye mali, cham kikadorora.
Kutokana na umuhimu wa chombo hiki na kutokana na pengo la
chombo chenye kukusanya wanamuziki wote na washiriki wengine kwenye muziki,
wakiwemo, wanamuziki, wachezaji( stage show), sound engineers wa studio na wa
muziki ‘live’, producers, managers na wadau wengine wa aina hiyo, imelazimika kukifufua tena chombo hiki muhimu. Lengo kuu la
mtandao huu ni kuwa chama cha wafanyakazi wanamuziki (Musicians Union). Chombo chenye kulea na kukuza
shughuli hii kuwa yenye taratibu zinazompasa mfanya kazi wa kazi hizi, kama inavyokuwa katika ulimwengu sehemu nyingine.Chombo hiki ni mwanachama hai wa Shirikisho la Wanamuziki Duniani (FIM).
Kwa sasa ajenda iliyo mbele ni bima ya afya ya wanamuziki. Si siri kuwa
tatizo la matunzo na huduma za wanamuziki na wafanyakazi wengine wa tasnia hii
ni gumu pale afya zao zinapokuwa na matatizo, hivyo tayari viongozi wameshakuwa
na mazungumzo ya awali na moja ya vyombo vya bima ya afya na kinachosubiriwa ni
wanamuziki kujiunga na chombo hiki ili kuweza kuanzisha taratibu hizi.
Pamoja na malengo haya Mtandao huu utaendesha semina na
warsha kwa ajili ya wanamuziki wanachama katika Nyanja mbalimbali za mambo ya
muziki. Katika kipindi hiki hiki tayari mtandao umewezesha wafadhili kufadhili
utafiti kuhusu matatizo yaliyomo katika biashara ya muziki jambo ambalo
litawezesha wafadhili kufadhili miradi itakayobuniwa katika kurekibisha hali
hiyo ngumu.
Tunakaribisha maombi ya uwanachama, unaweza kuonyesha nia
kwa kutuma jina na anwani yako katika inbox ya ukurasa facebook Wanamuziki wa Tanzania au kupitia
anwani ya musicnettz@yahoo.com na utaweza kuwapewa maelezo ya ziada. Tuma jina lao, jinsia,
mahala uliko, namba ya simu, anwani ya email na taaluma unayoshiriki, …. UMOJA
NI NGUVU
Subscribe to:
Posts (Atom)