Tuesday, March 25, 2014

MKUTANO WA KWANZA WA VIONGOZI WA BENDI WAFANYIKA BASATA


Mkutano wa kwanza wa viongozi wa bendi mwaka huu, uliofanyika katika ukumbi wa Basata Jumanne tarehe 25 March umekuwa na mengi mazuri. Kwanza wanamuziki walikumbushwa mengi ambayo yameshindikana kufanyika kwa kutokuweko na umoja wenye nguvu wa wanamuziki, hasa wa muziki ‘live’, hivyo kulipatikana azimio kuwa wanamuziki wahamasishane wenyewe kujiunga na vyama vya muziki. 
Maelezo pia yalitolewa kuhusu nafasi ya sanaa katika Katiba mpya na juhudi ambazo zimekwisha fanywa na jinsi zinavyohitaji umoja katika kipindi hiki cha Bunge la Katiba. Viongozi hawa hatimae walizungumzia changamoto mbalimbali ambazo zinaikumba tasnia hii, na kuamua kuanza kujipanga kupunguza matatizo yale ambayo yako katika uwezo wa bendi. Iliamuliwa kuweko na kikao kingine Jumanne ijayo kuanzia saa nne asubuhi palepale BASATA na kutafuta wajumbe wengine kutoka bandi ambazo hazikuhudhuria mkutano wa leo.






Wednesday, March 5, 2014

MTANDAO KUFANYA WARSHA YA VIONGOZI WA BENDI

Kamati ya uongozi ya Mtandao wa wanamuziki(TAMUNET), leo imefanya kikao na katika yaliyopangwa na kufanya warsha ya siku moja ya viongozi wa bendi kujadili changamoto mbalimbali zinazozikuta bendi katika zama za sasa. Tarehe ya warsha hii inategemea makubaliano na BASATA ambao watakuwa kiungo muhimu katika warsha hii. Lakini warsha hii lazima itakuwa mwezi huu March kabla ya mkutano mkubwa wa wanamuziki mara baada ya warsha hiyo.